Wananchi wa mtaa wa nyahanga mjini Kahama wakiangalia mwili wa kichanga hicho kilichowekwa kwenye mfuko.
Mwili wa mtoto mwenye
umri wa siku 1 umekotwa ukiwa umetupwa katika eneo la dampo la shule ya
msingi Nyahanga wilayani Kahama mkoani Shinyanga.
Mashuhuda watukio hilo
wamesema mwili wa mtoto huyo umegunduliwa jana na wanafunzi wa
shule ya msingi Nyahanga wakati wanaenda kutupa takataka kwenye dampo
hilo.
Akizungumzia tukio hilo
afisa mtendaji wa kata ya Nyahanga Nambo Ntaki amesema wananchi wa
mtaa huo wanapaswa kutoa ushirikiano ili kuweza kumbaini mtu ambaye
ametekeleza tukio hilo ambalo ni la kinyama.
Kwa upande wake
mwenyekiti wa mtaa huo Wiliam Upamba amesema kuwa wananchi wanapaswa
kukomesha matukio kama hayo ambayo yanaleta sifa mbaya kwenye jamii.
Mwili wa mtoto huyo
umekabidhiwa kwa viongozi wa mtaa wa nyahanga na jeshi la polisi
kwaajili ya taratibu za mazishi na kutoa wito kwa wananchi kushirikiana
jeshi la polisi kwa lengo la kumbaini mtu ambaye ametekeza tukio hilo.
Na Salvatory Kelvin - Kahama
Social Plugin