Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

Maskini!! MTOTO WA SIKU MOJA ATUPWA KWENYE JALALA HUKO KAHAMA

Wananchi wa mtaa wa nyahanga mjini Kahama wakiangalia mwili wa kichanga hicho kilichowekwa kwenye mfuko.

Mwili wa mtoto mwenye umri wa siku 1 umekotwa ukiwa umetupwa katika eneo la dampo la shule ya msingi Nyahanga wilayani Kahama mkoani Shinyanga.

Mashuhuda watukio hilo wamesema mwili wa mtoto huyo umegunduliwa jana na wanafunzi wa shule ya msingi Nyahanga wakati wanaenda kutupa takataka kwenye dampo hilo.

Akizungumzia tukio hilo afisa mtendaji wa kata ya Nyahanga Nambo Ntaki amesema wananchi wa mtaa huo wanapaswa kutoa ushirikiano ili kuweza kumbaini mtu ambaye ametekeleza tukio hilo ambalo ni la kinyama.


Kwa upande wake mwenyekiti wa mtaa huo Wiliam Upamba amesema kuwa wananchi wanapaswa kukomesha matukio kama hayo ambayo yanaleta sifa mbaya kwenye jamii.
Mwili wa mtoto huyo umekabidhiwa kwa viongozi wa mtaa wa nyahanga na jeshi la polisi kwaajili ya taratibu za mazishi na kutoa wito kwa wananchi kushirikiana jeshi la polisi kwa lengo la kumbaini mtu ambaye ametekeza tukio hilo.

Na Salvatory Kelvin  - Kahama

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com