Siku moja baada ya jeshi la polisi nchini kupiga
marufuku nyama vya siasa kuendelea kutoa mafunzo mbalimbali ya ukakamavu na
ulinzi kwa vijana, mwenyekiti wa chama cha Demokrasia na Maendeleo Taifa
(CHADEMA) Freeman Mbowe amepinga kauli hiyo.
Mbowe alisema kuwa ikiwa jeshi la polisi litaamua
kuwakataza kuendesha mafunzo hayo kwa vijana wao, ambayo alisema yanatolewa
mchana wataamua kutoa mafunzo usiku.
Kiongozi huyo alitoa kauli hiyo jana wakati
akifunga mafunzo ya vijana wapatao 200 katika wilaya ya Itilima Mkoani Simiyu,
ambapo alibainisha kuwa mafunzo hayo yanatolewa kwa vijana wao ni juu ya
uzalendo.
Aliongeza kuwa kitendo cha tamko la viongozi wa
jeshi hilo, ni woga wa chama Cha Mapinduzi pamoja na wivu kwa Chadema, kuona
wanaungwa mkono na mamia ya vijana nchi nzima kupata mafunzo hayo.
Social Plugin