Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

MIONGONI MWA WAPIGANAJI WA AL SHABAAB WALIOUA WANAFUNZI NI MTOTO WA AFISA WA SERIKALI YA KENYA

Wanafunzi wa chuo kikuu cha Garissa wakitoroka shambulio
Serikali ya Kenya imemtambua mmoja ya wapiganaji waliohusika katika mauaji ya chuo kikuu cha Garissa kwamba ni mtoto wa afisa wa serikali.
Msemaji wa wizara ya ndani amesema kuwa Abdirahim Abdullahi ni miongoni mwa watu wanne walioshambulia chuo kikuu cha Garissa siku ya Alhamisi na kuwaua watu 148.
Mtu huyo sasa ametambulika kama mwana wa kiume wa Chifu wa eneo la Kazikazini mashariki mwa Kenya.
Alidaiwa kutoweka na ilihofiwa kwamba amesafiri nchini Somalia.
Wizara ya ndani inasema kuwa wapiganaji wote waliuawa siku ya Alhamisi.
Washukiwa wengine watano wamekamatwa kufikia sasa kwa kuhusishwa na mauaji hayo ambayo ni mabaya zaidi kuwahi kutekelezwa na kundi la wapiganaji wa Alshabaab.
via>>BBC

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com