ANGALIA PICHA_UWANJA WA CCM KAMBARAGE UMEJAA MAJI MECHI YA SIMBA SC Vs KAGERA SUGAR IMEAHIRISHWA!!

Maji ya mvua yakiwa katika  goli la uwanja wa CCM Kambarage mjini Shinyanga-picha zote na Marco Maduhu-Malunde1 blog

 Pamoja na maji kujaa uwanjani,hata hivyo kulikuwa na mashabiki kiduchu hali ambayo wataalam wa mambo wanadai pengine pia imechangia kuahirishwa kwa mechi hiyo kwa kuhofia kukosa mapato

Mashabiki wa mpira wa miguu wakiwa jukwaa kuu
Mashabiki wakishangaa uwanjani baada ya mechi kuahirishwa

 
Maji yakiwa uwanjani

Mazingira uwanjani

Sehemu nyingine ya uwanja hakuna maji-picha zote na Marco Maduhu-Malunde1 blog


Mchezo wa ligi kuu Vodacoma Tanzania bara baina ya Kagera Sugar na Simba SC uliotakiwa kufanyika katika uwanja wa CCM Kambarage mjini Shinyanga umeahirishwa jioni hii kutokana na uwanja wa kujaa maji kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha mkoani Shinyanga.

Uongozi wa Chama cha mpira wa miguu mkoa wa Shinyanga umesema hali ya hewa nzuri hivyo mchezo huo utafanyika kesho kutwa siku ya Jumatatu.

Mwenyekiti wa Chama cha Mpira wa miguu mkoa wa Shinyanga Benister Lugola amesema mchezo utafanyika

Hata hivyo pamoja na maji kujaa katika uwanja huo hususani upande wa magoli ,mashabiki wa mpira wa miguu hawajajitokeza kwa wingi hivyo hali ambayo inatajwa kuwa imechangia kwa kiasi kikubwa kuahirishwa kwa mechi hiyo ingawa timu zote zilikuwa tayari kucheza,huku timu ya Simba ikipiga kelele zaidi kwani wanatumia gharama kubwa kutokana na kwamba kesho walitakiwa kuondoka mkoani Shinyanga. 

Wakizungumza na Malunde1 blog Mashabiki wamelalamikia kitendo cha mechi kuahirishwa kwani wengi wao wametoka nje ya mkoa wa Shinyanga huku  wakidai kuwa maji yalikuwa ya kawaida tu tena sehemu za magoli tu kwa maana hiyo hapakuwa na sababu ya kuahirisha na kuongeza kuwa tatizo ni maslahi kwani majukwaa hayakuwa na watu wa kutosha uwanjani hapo.

"Ukweli ni kwamba maji hayakuwa mengi sana,hapa wametafuta tu kisingizio,kwanza mvua ilikuwa imekatika,kwanini waahirishe mechi kirahisi rahisi tu hivi?",alifoka mmoja wa mashabiki hao.

Na Marco Maduhu-Malunde1 blog

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com
Previous Post Next Post