Mwanaume
mmoja katika kijiji cha Migosi, Kaunti ya Siaya, nchini Kenya amejiua
kwa kunywa sumu baada ya kugombana na mkewe kwa kile alichodai kuwa
alimpakulia ugali mdogo.
Mwanaume huyo Samuel Abuya, ambaye ni baba wa watoto kumi, alianza kugombana na mke wake kuhusu chakula muda mfupi baada ya kufika nyumbani akiwa amelewa.
Mtoto wake wa kiume David Ouma,
amesema baba yake aliwafukuza nyumbani baada ya mama yake kumpakulia
ugali na kuanza kulalamika kuwa ni mdogo na kutishia kujiua, baada ya
kufukuzwa walikimbilia kwa mjomba wao anayeishi jirani, lakini
aliwafuata na kuendelea kugombana ndipo mama yake alipomuuliza kwa nini
analalamika chakula kidogo wakati haachi hela ya chakula maneno
yaliyomkasirisha na kuondoka huku akitishia kujiua.
Waliporudi nyumbani saa tano usiku
walimkuta baba yao ameanguka chini akijigalagaza kwa maumivu, pembeni
yake kukiwa na chupa yenye dawa ya kuulia mchwa, walijaribu kuokoa
maisha yake kwa kumnywesha maziwa lakini hayakumsaidia akafariki.
Social Plugin