Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

ANGALIA PICHA AJALI_MAGARI MATATU YAGONGANA HUKO TANGA,WATU 10 WAFARIKI DUNIA!!


Name:  IMG-20150409-WA0004.jpg
Views: 0
Size:  92.1 KB
Watu 10 wamefariki dunia na 35 kujeruhiwa katika ajali iliyohusisha magari matatu katika eneo la Mkata kijiji cha Mbweni wilayani Handeni Mkoani Tanga majira ya saa 5 asubuhi ya leo.

Akizungumza na East Africa Radio Kamanda wa kikosi cha usalama barabara mkoa wa Tanga amesema kuwa ajali hiyo imehusisha mabasi mawili ya abiria na gari dogo katika barabara ya Dar es salaam kwenda Tanga na Arusha.

Kwa mujibu wa Kamanda gari dogo ilikuwa likitaka kulipita lori lililokuwa mbele yake na ndipo ilipogongana uso kwa uso na basi la Ratco lililokuwa likitokea Tanga kwenda Dar es salaam.

Baada ya Basi la Ratco kugonganana na gari dogo, lilipoteza mwelekeo na kugongana tena uso kwa uso na basi la Ngorika lililokuwa likitokea Dar es salaam kwenda Arusha.

Aidha kamanda huyo amesema kuwa kati ya watu 10 waliofariki dunia wanaume watano wakiwemo dereva wa gari dogo na dereva wa basi la Ngorika pamoja na wanawake watano wakiwemo watoto wawili.

ANGALIA PICHA KUTOKA ENEO LA TUKIO HAPA CHINI
Wananchi wakiwa eneo la tukio


Name:  IMG-20150409-WA0003.jpg
Views: 0
Size:  149.7 KB


Name:  IMG-20150409-WA0005.jpg
Views: 0
Size:  110.3 KB

 
Mungu azilaze roho za marehemu mahali pema peponi

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com