Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

Picha: ASKOFU MTEULE LIBERATUS SANGU ASIMIKWA RASMI KUWA ASKOFU WA JIMBO KATOLIKI LA SHINYANGA,PICHA ZIKO HAPA TUKIO ZIMA


Askofu mteule wa jimbo katoliki la Shinyanga Mosinyo Liberatus Sangu leo Aprili 12,2015 amewekwa wakfu na kusimikwa rasmi kuwa Askofu wa jimbo hilo lililokuwa wazi kwa muda wa miaka mitatu tangu askofu aliyekuwa analiongoza Aloysius Balina kuaga dunia mwaka 2012. 

Ibada ya kuwekwa wakfu na kusimikwa kwa askofu mpya wa kanisa katoliki jimbo la Shinyanga Liberatus Sangu imefanyika katika kanisa kuu la Mama Mwenye Huruma la Ngokolo mjini Shinyanga ikiongozwa na askofu wa jimbo kuu la Dar es salaam mwadhama Polycarp Kadinali Pengo ambapo rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Jakaya Kikwete alikuwa mgeni rasmi.

Maelfu ya watu wameshuhudia tukio hilo muhimu wakiwemo mapadre,watawa,waumini,wabunge,mawaziri,wakuu wa wilaya,wakuu wa mikoa,viongozi wa vyama vya siasa,viongozi wa dini dini mbalimbali na watu mbalimbali wenye mapenzi mema.

Askofu Liberatus Sangu anakuwa askofu wa nne katika jimbo la Shinyanga,wa kwanza alikuwa Askofu Mc Gurkin Eduard kuanzia 3.10.1956 hadi 1975,wa pili ni askofu Castor Sekwa,ambaye ni askofu wa kwanza mzalendo mwaka 1975-1996,wa tatu ni askofu Aloysius Balina kuanzia 16.11.1997 hadi 06.11.2012.

Angalia hapa chini Matukio katika picha.....Picha zote na Kadama Malunde-Malunde1 blog
Kulia ni waziri mkuu mstaafu Edward Lowassa akiwasili katika kanisa la Mama Mwenye Huruma la Ngokolo mjini Shinyanga leo,kushoto kwake ni mwenyekiti wa CCM mkoa wa Shinyanga Khamis Mgeja
Baada ya kuwasili wanafurahia jambo 
Askofu Pengo akiongoza ibada ya kuwekwa wakfu na kusimikwa kwa askofu Liberatus Sangu,kushoto kwake ni aliyekuwa msimamizi wa kitume wa jimbo la Shinyanga tangu mwaka 2012 Askofu Yuda Thadeus Ruwaich kutoka jimbo katoliki la Mwanza
Nje ya kanisa 
Maaskofu na mapadre wakiwa eneo la tukio wakati wa ibada(wa pili kutoka kulia mstari wa kwanza ni askofu Sangu 
Wakakwaya wakifanya yao 
Askofu mteule Sangu akijibu maswali kabla ya kusimikwa rasmi kuwa askofu wa jimbo katoliki la Shinyanga 
Askofu Sangu akiwa amejilaza chini wakati ibada hiyo
Askofu Sangu akiwa amelala chini 
Askofu Sangu akiwekewa mikono na maaskofu kutoka maeneo mbalimbali nchini Tanzania 
Balozi wa Papa nchini Francisco,Padilla akimwekea mikono askofu Sangu 
Askofu Sangu akiwekewa kitabu cha injili kichwani 
Askofu Sangu akipakwa mafuta 
Askofu Sangu akikabidhiwa kitabu cha injili 
Askofu Sangu akivalishwa pete ya uaskofu 
Ibada inaendelea 
Askofu Sangu akikabidhiwa bakora ya kiaskofu 
Ibada inaendelea 
Viongozi mbalimbali wakiwa eneo la tukio 
Viongozi mbalimbali wakipeana mkono na askofu Sangu 
Waziri mkuu mstaafu Edward Lowassa akipeana mkono na Askofu Sangu 
Maaskofu wakiwa katika picha ya pamoja baada ya askofu Sangu kuwekwa wakfu na kusimikwa rasmi 
Askofu Sangu akiwa na machifu 
Askofu Sangu katikati akiwa katika kiti cha uaskofu 
Ibada ya kusimikwa kwa askofu Sangu ikiendelea,rais Kikwete (wa tatu )akiwa eneo la tukio muda mfupi baada ya kuwasili 
Rais Kikwete akisaini 
Watangazaji wa Radio Faraja fm Stereo,inayomilikiwa na kanisa katoliki Shinyanga wakirusha matangazo ya moja kwa moja kutoka eneo la tukio,aliyeshikilia kipaza sauti ni Ndugu Anikazi Kumbemba 
Rais Kikwete akifuatilia kilichokuwa kinajiri eneo la tukio,wa kwanza kushoto ni mkuu wa mkoa wa Shinyanga Ally Nassoro Rufunga,wa kwanza kulia ni mkuu wa wilaya ya Shinyanga bi Josephine Matiro,akifuatiwa na mwenyekiti wa CCM mkoa wa Shinyanga ndugu Khamis Mgeja 
Rais Kikwete akitoa salamu za serikali kwa askofu Askofu ambapo alimpongeza kwa kuteuliwa kuwa askofu wa jimbo katoliki la Shinyanga
Picha zote na Kadama Malunde-Malunde1 blog

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com