Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

Noma! ASKOFU GWAJIMA AHOJIWA NA POLISI KWA MASAA MATANO,MASWALI MENGI HAYANA UHUSIANO NA ASKOFU PENGO


 

Askofu wa  Kanisa la Ufufua na Uzima Josephat Gwajima amelitikisa  tena  Jiji la Dar es Salaam leo  mara   baada  kuwasili makao  makuu  ya  Jeshi la polisi kanda maalum ya Dar es Salaam ili  kuendela  na  mahojiano kuhusu tuhuma za kumkashfu  Askofu Pengo.
 
Gwajima amewasili leo Kwenye Makao Makuu ya Jeshi la polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam Majira ya saa mbili kamili asubuhi huku akisindikizwa na viongozi mbali mbali wa Kanisa la Ufufuo na Uzama pamoja na Mwanasheria wake .

Eneo  lote  la  kituo  hicho  cha  polisi  lilikuwa  chini  ya  ulinzi  mkali wa maofisa mbalimbali wa Usalama wa Taifa wakisaidiwa na Jeshi la Polisi.
 
Baada  ya  kuwasili  kituoni  hapo, umati mkubwa  wa Waumini wake ulizunguka  maeneo yote ya  Kituo hicho   huku  wengine  wakiwa maeneo ya stendi ya Treni ya Reli ya kati.

Kama  kawaida, Waumini  hao walikuwa  wakiimba nyimbo mbalimbali ambazo wanadai zilikuwa  mahususi  kumpa nguvu Askofu huyo ajipu kesi hiyo kwa ufasaha.
 
Baada  ya  Mahojiano  ya  takribani  masaa  Matano, hatimaye   Askofu Gwajima  alitoka  ndani  ya kituo  hicho,lakini  katika  hali  isiyo  ya  kawaida,Askofu  huyo  aligoma kuongea na vyombo vya habari.
 
Baada  ya  Gwajima  kugoma  kuongea,mwandishi wetu  alimfuata Mwanasheria  wake  aliyekuwa  ameambatana  naye,Paul Mallya ambaye alisema kuwa  mteja  wake  alikuwa  amechoka, hivyo  asingeweza  kuongea.

Mallya  alimweleza  mwandishi kuwa  mambo aliyohojiwa  Gwajima  leo  ni kuhusu mali zake na sio matamshi ya kumtukana Askofu  Pengo.
 
Askofu kahojiwa maswali mengi tena sio ya kuhusu kumtukana Askofu Pengo.Wametaka hati ya Helikopta yake anayomiliki,hati za kanisa lake  na hati za viwanja vyake   ambavyo  ameambiwa  avipeleke  wiki  ijayo,”alisema Mwanasheria Mallya.

Mallya aliongeza kuwa kutokana na Afya ya  mteja  wake  kuwa mbaya , mahojiano yake yameahirishwa hadi  wiki  ijayo.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com