|
Kumetokea ajali ya aina yake leo jioni majira ya saa 12 mjini Shinyanga ambapo gari ndogo aina ya Suzuki Escudo yenye namba za usajili T128 ASZ (Pichani) ikiendeshwa na mtu mmoja aliyejukana kwa jina la Ezekiel fundi magari limetumbukia katika daraja lisilo kuwa na kingo la Buluba katika barabara ya Magadula inayotenganisha kata ya Ngokolo na Ndembezi katika manispaa ya Shinyanga-Picha zote na Kadama Malunde-Malunde1 blog
|
|
Gari likiwa ndani ya maji
|
|
Mashuhuda wa tukio hilo waliozungumza na Malunde1 blog
ilifika eneo la tukio haraka kama kawaida yake wamesema dereva wa gari hiyo
ambaye ni fundi magari alikuwa katika mwendo kasi hali ambayo ilimshinda gari
nan kutumbukia kwenye mto unaopita katika daraja hilo.
|
Wakazi wa Shinyanga wakiwa eneo la tukio.
Mwandishi wa habari kutoka Radio Faraja Moshi Ndugulile akitafakari jambo katika daraja la Buluba.
Gari likiwa ndani ya mto kwenye daraja la Buluba lisilokuwa na kingo hali ambayo imekuwa ikilalamikiwa na wakazi wa eneo hilo kwani mto ni mkubwa hivyo kuhatarisha maisha ya watumiaji wa daraja hilo hasa kipindi cha mvua na nyakati za usiku.Taarifa tulizozipata ni kwamba watu wengi sana wamekuwa wakitumbukia katika mto huo(daraja) pamoja na daraja jingine lililoko jirani na Moleka Hotel ambako mto huo pia unapita
|
Malunde1 blog imeambiwa kuwa katika gari hilo kulikuwa na
watu wawili na hakuna aliyepoteza maisha na walitolewa kupitia kwenye dirisha
la gari hiyo upande wa juu na wasamaria wema wakiwemo waendesha baiskeli
maarufu “daladala”.
|
|
Inaelezwa kuwa fundi gari huyo alikuwa anatoka eneo la
Empire Hotel akiendesha gari kwa mbwembwe kuelekea kwenye gereji iliyoko Ngokolo mjini Shinyanga na
alionekana kunyumba kabla ya kutumbukia kwenye mto huo.
|
|
Askari
wa usalama barabarani akiwa eneo la tukio |
|
Mashuhuda wa tukio hilo wakizungumza mbele ya askari wa
usalama barabani eneo la tukio.
|
Mashuhuda wa tukio hilo wakizungumza mbele ya askari wa usalama barabani eneo la tukio.
|
Gari ikiwa ndani ya maji |
|
Askari
wa usalama barabarani wakifanya yao eneo la tukio |
|
Upande
wa pili wa daraja la Buluba ambalo halina kingo na kuhatarisha maisha ya
watumiaji wa barabara hiyo. |
|
Askari wa usalama barabarani wakipima eneo la ajali |
|
Eneo la tukio |
|
Gari likiwa ndani ya mto kwenye daraja la Buluba lisilokuwa na kingo hali ambayo imekuwa ikilalamikiwa na wakazi wa eneo hilo kwani mto ni mkubwa hivyo kuhatarisha maisha ya watumiaji wa daraja hilo hasa kipindi cha mvua na nyakati za usiku.Taarifa tulizozipata ni kwamba watu wengi sana wamekuwa wakitumbukia katika mto huo(daraja) pamoja na daraja jingine lililoko jirani na Moleka Hotel ambako mto huo pia unapita.Shikamoo Uongozi wa Manispaa ya Shinyanga!!-Picha zote na Kadama Malunde-Malunde1 blog |
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com
Social Plugin