Ukatili aliyofanyiwa Hanafi Daudi (31) ambaye ni mkazi wa Salasala Kilimahewa jijini Dar es Salaam, yupo katika hali mabaya baada ya kumwagiwa mafuta ya moto yaliyokuwa jikoni yakikaangia chipsi alifanyiwa kitendo hicho baada ya kwenda kukopa chipsi kwa muuzaji wa kibanda hicho.
Akifanya mahojiano na Mwandishi wa habari hizi alikuwa na haya ya kusema
“Ilikuwa
usiku wa saa 3:30 hivi, muda ambao watu walikuwa wanaangalia mpira.
Ndipo nilipoamua kwenda pale kwa lengo la kuomba kukopeshwa chipsi kwa
kuwa sikuwa na pesa muda huo. Niliamini ningemlipa kesho yake"
“Nilipofika,
yule jamaa nilimuona kama yuko tofauti hivi lakini nikaamua nimuombe
anisaidie kwa muda ule. Nikashangaa tu akanyanyua karai la mafuta ya
chipsi na kunimwagia usoni.Nilihisi kuchanganyikiwa, nikakimbia mpaka
kwa wenzangu. Wakati huo macho yote yalikuwa yameziba, sioni kitu
chochote. Ndipo wenzangu wakanibeba na kunileta hapa Muhimbili kwa
msaada wa usafiri njiani,”
“Wale
wenzangu baada ya kunifikisha hapa na kuondoka sijawaona tena mpaka
leo. Sina msaada wowote, sina ndugu wa kunisaidia, sina mawasiliano na
watu wa nyumbani Tanga.
“Najisikia
vibaya sana kwa sababu mtuhumiwa alikimbia muda uleule aliponifanyia
ukatili huu. Kikubwa ninamwomba Mungu anisaidie kwani yeye ndiye
anayejua cha kunifanyia.”
via>>GPL |
Social Plugin