Mamia
ya wakazi wa wilaya za Kilosa na Kilombero wamejitokeza katika mazishi
ya pamoja ya watu 15 kati ya 19 waliofariki katika ajali ya basi ya
Nganga ambalo liligongana na fuso kisha kuwaka moto katika eneo la Iyovi
na kuzikwa katika kaburi la pamoja kwenye makaburi ya Msamvu Ruaha
wilayani Kilosa mkoani Morogoro.
Akizungumza
kwa niaba ya serikali ya mkuu wa wilaya ya Kilosa John Henjewele
amesema serikali imewalazimu kufanya mazishi ya pamoja ya watu
waliofariki kwenye ajali hiyo ambao miili yao haijatambulika.
Pia
amesema serikali itaendelea na zoezi la ukaguzi wa magari mkoani wa
Morogoro ili kudhibiti ajali za mara kwa mara na kupoteza maisha ya watu
huku wengine wakiachwa na vilema vya maisha.
Naye mkuu wa wilaya ya Kilombero Lephy Gembe amewataka wananchi kuwa na uvumilivu katika msiba mkubwa walioupata.
Kwa
upande wake diwani wa kata ya Ruaha Rahel Nyangasa amesema wamepokea
msiba huo kwa masikitiko makubwa kwani umekuwa ni pigo kubwa kwa wakazi
wa wilaya hizo.
Ndugu
na waombolezaji nao wamesema msiba huo si wakusahaulika kwani
umewashtua sana na muinjilisti wa kanisa la kiinjili la kilutheri Issaya
Chura akiomba serikali kuendelea kukabiliana na madereva wabovu.
Social Plugin