Jana April 7 ilikuwa siku ya tatu ya maombolezo baada ya shambulio la kigaidi Chuo Kikuu cha Garissa Kenya, watu waliweka misalaba na mishumaa katika viwanja vya Nairobi kuwakumbuka wanafunzi 148 waliouawa katika shambulio hilo.
Wanafunzi wa Chuo cha Garissa walifanya maandamano Nairobi wakiwa na ujumbe kuishinikiza Serikali ya Kenya kuimarisha ulinzi.
Zaidi ya watu 2000 walikusanyika kulaani mashambulizi hayo huku Mahakama kuu ikitoa mwezi mmoja kwa Polisi kuwahoji watu sita waliokamatwa mpaka sasa kwa kuhusika na tukio hilo ambapo kati yao anatajwa kuwepo Mtanzania mmoja.
Kenya imefungia account za Benki za watu 86 ambao wanahisiwa kukisaidia Kikundi cha Al-Shaabab.