Kutoka Dar es Salaam leo April 28 2015
kingine ambacho kimechukua nafasi kubwa kwenye HEADLINES ni hii stori
ya uzinduzi wa Meli kubwa mbili za Kivita ambazo zimezinduliwa na Rais Kikwete.
Meli zimekabidhiwa kwa Kikosi cha Jeshi la Maji TZ Kigamboni.. Hapa unaweza kuona picha kutoka kwenye uzinduzi wa Meli hizo.
Meli hizi zitakuwa zikitumiwa kwenye patrol katika eneo la Bahari.
Amiri Jeshi Mkuu Rais
Jakaya Mrisho Kikwete akizindua rasmi meli mbili za doria bahari kuu TNS
Msoga na TNS Mwitongo kwenye sherehe zilizofanyika Kamandi ya Jeshi la
Maji Kigamboni jijini Dar es salaam leo April 28, 2015.
Amiri Jeshi Mkuu Rais
Jakaya Mrisho Kikwete akikagua mara baada ya kuzindua rasmi meli vita
mbili za doria bahari kuu TNS Msoga na TNS Mwitongo kwenye sherehe
zilizofanyika Kamandi ya Jeshi la Maji Kigamboni jijini Dar es salaam
leo April 28, 2015
Amiri Jeshi Mkuu Rais
Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na Chifu Edward Wanzagi wa kabila la
Wazanaki (kati) pamoja na Mbunge wa Afrika Mashariki Mhe Makongoro
Nyerere baada ya kuzindua rasmi meli vita mbili za doria bahari kuu TNS
Msoga na TNS Mwitongo kwenye sherehe zilizofanyika Kamandi ya Jeshi la
Maji Kigamboni jijini Dar es salaam leo April 28, 2015.
Picha zote kutoka: Ikulu, issamichuzi.blogspot.com na tanzaniangovernment.blogspot.com.