Maadhimisho ya siku
ya wafanyakazi duniani(Mei Mosi) katika mkoa wa Shinyanga yatafanyika Kesho katika
uwanja wa Uhuru uliopo katika mgodi wa
Mwadui wilayani Kishapu.
Mwenyekiti wa Vyama Huru vya
Wafanyakazi –TUCTA mkoa wa Shinyanga Fue Mrindoko(Pichani) amesema sherehe hizo zitaanza
saa moja asubuhi kwa maandamano kutoka
jengo la Maendeleo vilivyopo katika mgodi wa Mwadui kuelekea kwenye uwanja wa
Uhuru uliopo katika mgodi huo.
Mrindoko amesema
mgeni rasmi katika sherehe hizo za Mei Mosi zitakazofanyika kesho Ijumaa
anatarajiwa kuwa mkuu wa mkoa wa Shinyanga Ally Nassoro Rufunga.
Amewataka wananchi
kujitokeza mapema na kwa wingi katika sherehe hizo ambazo zitahudhuriwa na
makundi mbali ya wafanya kazi wa serikali,mashirika ya Umma na Taasisi binafsi.
Mrindoko amesema
katika sherehe hizo pia kutakuwa na burudani mbalimbali ikiwemo mashindano ya mbio
za baiskeli,ngoma,bendi na kuvuta kamba.
Amesema kauli mbiu ya
Maadhimisho hayo nchini Tanzania mwaka huu ni “Mfanyakazi Jiandikishe Kura Yako Ina Thamani
Kwa Maendeleo Yako”.
Na Kadama Malunde-Malunde1 blog