Leo Alhamis,Aprili 2,2015 afisa mtendaji mkuu wa Diamond Trust Bank Tanzania Limited(DTB) bi Nasim Devj amezindua tawi jipya la benki hiyo lililopo katika barabara ya Ngaya/Isaka mjini Kahama mkoani Shinyanga,ambapo watu mbalimbali kutoka ndani na nje ya Tanzania wamehudhuria uzinduzi huo.Tawi la Kahama ni la tatu katika kanda ya Ziwa(mengine yapo Mwanza na Tabora) lengo likiwa ni kuhudumia jamii ya wafanyabiashara nchini Tanzania--picha zote na Kadama Malunde-Malunde1 blog
Diamond Trust Bank Tanzania Limited(DTB) hivi sasa ina matawo 23 ikiwa na mpango wa kufungua matawi matatu zaidi kabla ya mwisho wa mwaka 2015,ambapo matawi mengi zaidi yanatarajia kufunguliwa katika miji ya Singida,Musoma na Kigoma.
Kushoto ni afisa mtendaji mkuu wa Diamond Trust Bank Tanzania Limited(DTB) bi Nasim Devij akizungumza jambo na wafanya kazi wa Benki hiyo kabla ya ufunguzi
Wafanyakazi wa Diamond Trust Bank kabla ya ufunguzi
Wageni waalikwa wakiendelea kuwasili katika benki hiyo kabla ya ufunguzi
Wageni waalikwa wakiwa katika eneo la tukio
DTB inakuwa benki ya 10 ya kibiashara kufungua milango yake katika wilaya ya Kahama huki ikitoa huduma kamili za kibenki kwa watu wa Kahama
Wageni mbalimbali kutoka nchini Kenya na Dar es salaam Tanzania
Mkurugenzi wa DTB Tanzania bwana Mehboob Champsi akizungumza wakati wa sherehe za Ufunguzi wa Tawila DTB mjini Kahama ambapo alisema mbali na kuwa na huduma nzuri za kibenki pia madhari ya benki hiyo yanavutia sana
Mkurugenzi wa DTB Tanzania bwana Mehboob Champsi alisema benki ya DTB inakua kwa kasi nchini Tanzania kutokana na maelezo ya kibiashara yanayokua na kutokana na ukuaji wa matandao wa matawi yao ambapo kwa mwaka 2014 benki imepata ongezeko la faida la asilimia 25 na kuwa na Tzs 20.09 bilioni ya pato kabla ya kodi,ikilinganishwa na pato la Tzs 16.13 bilioni mwaka 2013.
Mkurugenzi wa DTB Tanzania bwana Mehboob Champsi alisema akiba za wateja zimekua kwa asilimia 44.5 kutoka Tzs 399.7 bilioni mwaka 2013 hadi Tzs 577.5 bilioni,wakati mali za benki zimefikia Tzs 690.0 bilioni ikionesha ukuaji wa asilimia 36.4 kwa mwaka 2014 kutoka Tzs 505.7 bilioni kwa mwaka 2013
Afisa mtendaji mkuu wa Diamond Trust Bank Tanzania Limited(DTB) bi Nasim Devji akizungumza wakati wa uzinduzi wa tawi la DTB Kahama ambapo alisema hivi sasa DTB hivi sasa ina matawi 23 nchi nzima,matawi 10 yapo jijini Dar es salaam,mawili yapo jijini Arusha.
Alisema matawi mengine yapo Mwanza,Zanzibar,Dodoma,Tanga,Mbeya,Moshi,Iringa,Morogoro,Tabora,Kahama na Mtwara
Sherehe za uzinduzi zinaendelea
Afisa mtendaji mkuu wa Diamond Trust Bank Tanzania Limited(DTB) bi Nasim Devji akizungumza wakati wa uzinduzi wa DTB Kahama
Wageni kutoka Dar es salaam na nchini Kenya
Mkurugenzi wa DTB Tanzania bwana Mehboob Champsi akikabidhi zawadi kwa wadau muhimu walifanikisha ujenzi wa Tawi la DTB Kahama
Afisa mtendaji mkuu wa Diamond Trust Bank Tanzania Limited(DTB) bi Nasim Devji akitoa zawadi kwa wadau walifanikisha ujenzi wa tawi la DTB Kahama
Katikati ni bi Sheribanu Kurji ambaye ni mama mzazi wa
afisa mtendaji mkuu wa Diamond Trust Bank Tanzania Limited(DTB) bi Nasim Devji akipokea zawadi ya kufanikisha ujenzi wa DTB tawi la Kahama
Uongozi wa DTB Kahama ukipokea zawadi maalum katika sherehe hizo za uzinduzi wa tawi la DTB Kahama
Bi Sheribanu Kurji ambaye ni mama mzazi wa afisa mtendaji mkuu wa Diamond Trust Bank Tanzania Limited(DTB) bi Nasim Devji akikata utepe kuashiria uzinduzi wa tawi la DTB Kahama
Utepe umekatwa
Ndani ya Benki_afisa mtendaji mkuu wa Diamond Trust Bank Tanzania Limited(DTB) bi Nasim Devji akimwongoza mama yake mzazi bi Sheribanu Kurji ambaye ni mama mzazi wa kuangalia ofisi mbalimbali za benki hiyo
Hapa ni katika ofisi ya meneja wa benki ya DTB Kahama
Ndani ya ofisi ya meneja wa DTB Kahama
KEKI WAKATI WA UZINDUZI WA DTB KAHAMA
Zoezi la kukata keki likiongozwa na bi Sheribanu Kurji ambaye ni mama mzazi wa afisa mtendaji mkuu wa Diamond Trust Bank Tanzania Limited(DTB) bi Nasim Devji
Zoezi la kukata keki linaendelea
Afisa mtendaji mkuu wa Diamond Trust Bank Tanzania Limited(DTB) bi Nasim Devji akimlisha keki meneja wa tawi la DTB Kahama bi Mercy Stephen
Ndani ya benki ya DTB Kahama
Wageni waalikwa wakifuatilia kilichokuwa kinaendelea katika benki hiyo
Ndani ya DTB Kahama
Mkurugenzi wa Malunde1 blog Ndugu Kadama Malunde akiwa na afisa mtendaji mkuu wa Diamond Trust Bank Tanzania Limited(DTB) bi Nasim Devji
Mwandishi wa gazeti la Nipashe ndugu Mohab Dominic akiwa na afisa mtendaji mkuu wa Diamond Trust Bank Tanzania Limited(DTB) bi Nasim Devji
Meneja wa tawi la DTB Kahama bi Mercy Stephen akizungumza katika uzinduzi wa huo ambapo aliwataka wakazi wa Kahama kutumia fursa ya benki hiyo kujiendeleza kibiashara
Wadau wakifuatilia kilichokuwa kinajiri
Meneja wa tawi la DTB Kahama bi Mercy Stephen akizungumza katika sherehe hizo za uzinduzi wa tawi la DTB Kahama
Wafanyakazi kutoka Submarine Hotel wakiwa eneo la tukio ambapo kila aliyehudhuria sherehe hizo alipata chakula kizuri kutoka hotel hiyo ya mjini Kahama
Wafanyakazi wa Submarine hotel wakifanya yao wakati wa sherehe hizo leo
Picha zote na Kadama Malunde-Malunde1 blog
Social Plugin