Gori lililofungwa kwa penati na kuipatia Simba ushindi,likifungwa na Ibrahim Hatibu katika kipindi cha pili dakika ya 68-picha zote na Marco Maduhu-Malunde1 blog |
Mashabiki wa Simba sc wakiwa na furaha baada ya kuibamiza Kagera Sugar 2-1 |
mashabiki wakiwa jukwaa kuu wakishuhudia mechi
MC Maarufu nchini Tanzania ICE akiwa juu ya gari la matangazo akifanya yake uwanjani
Mchezo unaendelea picha zote na Marco Maduhu-Malunde1 blog
Timu ya Simba SC klabu imeibamiza bao 2-1 timu ya Kagera Sugar katika mchezo wa ligi kuu Vodacom Tanzania bara uliofanyika katika uwanja wa CCM Kambarage mjini Shinyanga,ambapo Kagera Sugar ilikuwa inatumia uwanja huo kama uwanja wa nyumbani.
Simba SC imejipatia goli la kwanza kipindi cha pili katika dakika ya 49 kupitia kwa mchezaji wake Ramadhani Singano,dakika ya 61 Kagera Sugar wakasawazisha kupitia kwa mchezaji wake Rashid Mandawa aliyeachia shuti kali lililomshinda golikipa wa Simba sc Peter Manyika.
Katika dakika ya 68 Ibrahimu Hatibu akaipatia Simba bao la pili kwa njia ya penati ambapo golikipa wa Kagera Sugar Aghton Anthony alishindwa kuifuta.
Katika dakika ya 68 Ibrahimu Hatibu akaipatia Simba bao la pili kwa njia ya penati ambapo golikipa wa Kagera Sugar Aghton Anthony alishindwa kuifuta.
Mtanange huo ulitarajiwa kufanyika siku ya Jumamosi iliyopita lakini kutokana na hali ya hewa kuwa mbaya baada ya maji kujaa uwanjani mchezo uliahirishwa.
Na Marco Maduhu-Malunde1 blog
Na Marco Maduhu-Malunde1 blog
Social Plugin