Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

Ubaguzi!! SHUHUDIA PICHA NA VIDEO JINSI MZUNGU ALIVYOFANYA MAUAJI YA MTU MWEUSI


Walter-Scott-2-600x313
Marehemu Walter Scott


Ni kama dunia ilianza kusahau matukio ya ubaguzi wa rangi, ishu ikarudi kuanza kuzungumziwa tena mwaka 2014 baada ya matukio ya watu wawili kuuawa mfululizo na Askari Marekani.

Leo hii ni story ya Afisa mwingine wa Polisi wa jimbo la CarolinaKusini kushtakiwa kwa mauaji, ushahidi wa video unaonesha Askari huyo alimpiga risasi nane mgongoni mtu ambae ni Mmarekani  mweusi.

Tukio hilo limetokea Jumamosi April 4 2015 ambapo shahidi mmoja alirekodi tukio hilo kwa video inayomuonesha Marehemu Walter Scott ambaye umri wake ni miaka 5o akikimbizwa na Afisa wa Polisi mzungu aliyekuwa na bunduki, akampiga risasi nane mgongoni, Walter alipoanguka alimfunga pingu.
screen-shot-2015-04-07-at-3-43-02-pm
Walter Scott akimkimbia Polisi

Afisa huyo Thomas Slager amejitetea kuwa Mmarekani huyo mweusi alikuwa akiendesha gari, alipomsimamisha kwa ajili ya kukaguliwa, alionekana kupingana na amri ya Polisi, akamuibia Polisi kifaa chake ambacho huwa Askarii wanakitumia kuwapiga shoti ya umeme wahalifu, Askari huyo akaamua kumpiga risasi.
scw
Walter Scott akifungwa pingu na Polisi

Hata hivyo Thomas Slager ameshtakiwa kwa mauaji na anakabiliwa na adhabu ya kifo au kifungo cha miaka 30 jela.
ws_21d713ac97c0ce379d3b23a3adcae87d
Thomas Slager akipandishwa kizimbani

Tazama video ya tukio hilo kwa kubonyeza play hapa chini…

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com