Tukio la mauaji ya limetokea Mbeya, inahusu tukio la mwanaume mmoja kumuingila kinguvu mtoto wa miaka 8.
Mwanaume
huyo alimuita msichana na kumuagiza dukani akamnunulie mafuta,
aliporudi alimuingilia kinguvu, akamuua halafu akautupa mwili wake
kwenye shimo.
Mama
wa mtoto huyo amesema alirudi mwenye mizunguko yake lakini hakumkuta
mtoto huyo, akaanza kumtafuta.. alipowauliza wenzake walisema alikuwepo
nyumbani baada ya kurudi shuke lakini hawajui baada ya hapo alielekea
wapi.
Akaamua
kutoa taariifa Polisi na kwa Balozi wa nyumba kumi, wakaitisha kikao..
baadae vijana wakaanza kumtafuta na kukuta mwili wake ukiwa kwenye
shimo.
Baada
ya siku tatu wanakijiji walianza msako na kukuta baadhi ya vitu vya
marehemu nyumbani kwa mwanaume mmoja zikiwemo nguo pamoja na damu, kwa
hasira wakaanza kumshambulia kwa kipigo na kuchoma moto nyumba hiyo hadi
Polisi walipofika na kuwazuia.
Polisi walimchukua mtuhumiwa huyo na kumpeleka kituoni.
Social Plugin