Watu
wawili wamejeruhiwa vibaya na kunusurika kufa akiwemo askari mgambo
baada ya kupata kipigo kutoka kwa wananchi wakati walipokuwa wakibomoa
nyumba ya mkazi mmoja aliyejulikana kwa jina la Ramadhani Husseni hali
iliyosababisha jeshi la polisi kuingilia kati katika eneo la Kinondoni
Manyanya jijini Dar es Salaam.
Katika tukio hilo ITV imeshuhududia kundi la watu likibomoa nyumba
hiyo na kutoa vitu nje huku askari wa mgambo wakiwa wanasimamia zoezi
hilo ambapo, baada ya kukamika kwa zoezi hilo wananchi wa maeneo hayo
waliwavamia baadhi ya vijana walikuwa wakibomoa nyumba hiyo na kuanza
kuwashumbulia kwa mawe na zana mbalimbali bila ya kupata msaada wa
kuokolewa hali iiyosababisha baadhi ya magari kuvunjwa vioo na baadhi ya
wafantyabiashara kulazimika Kufunga maduka.
Akizungumza na waandishi wa habari mmoja wa wamiliki wa nyumba hiyo
bwana Ramadhani Husseni amesema wanashangazwa na kikundi hicho kuvamia
na kubomoa nyumba hiyo wakati mahakama kuu ilishatoa hukumu kwa wao
wanahaki ya kumiliki nyumba hiyo kisheria.
Kwa upande wake mmoja wa wakazi katika nyumba hiyo amelalamikia
kikundi hicho kuvamia vyumba vya wapangaji kubomoa bila la kushirikisha
uongozi wa serikali ya mtaa na kuiba fedha na vifaa mbalimbali.
via>>ITV
Social Plugin