Wanachama
Saba (7) wa klabu ya Simba ya Dar es salaam kutoka tawi la Mpira na
Maendeleo (maarufu kama Simba UKAWA) ambalo limewahi kutangazwa kufutwa
wamefariki dunia katika ajali ya basi mkoani Morogoro.
Wanachama
hao wakiwa katika basi lao walikuwa wakielekea Shinyanga kwa ajili ya
kuipa nguvu Simba ambayo inatarajiwa kushuka katika dimba la CCM
Kambarage kuikabili Kagera Sugar katika mchezo wa ligi Kuu Tanzania Bara kesho..
Vifo hivyo vimefikia 7 baada ya watano kufa palepale na wengine wawili
waliokuwa majeruhi kufariki katika hospitali ya mkoa wa Mororgoro.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro SACP Leonard Paul amethibitisha
habari hizi na kusema kuwa majeruhi wamebaki 13 na kufanya vifo kufikia
saba hadi majira ya saa 2 usiku wa April 03,2015.
ANGALIA PICHA ZA AJALI HIYO HAPA
ANGALIA PICHA ZA AJALI HIYO HAPA
Social Plugin