Idadi
kubwa ya watu waliokuwa wanasafiri kati ya Bariadi ,Meatu ,Shinyanga
na Arusha wamekwama kwa zaidi ya saa kumi katika kijiji cha Mwakasubi Kisesa baada ya maji kujaa katika mto Mdala na kusitisha mawasiliano ya
barabara hiyo huku baadhi ya watu waliolazimisha kuvuka wakinusurika
kufa kwa maji.
Wakizungumza katika eneo la tukio watu waliokutwa na adha hiyo
wamesema hali hiyo inatokana na miundombinu mibovu ya barabara na
madaraja na imewasababishia mateso makubwa kwani baadhi yao walikuwa
wanafuata huduma muhimu wanakoenda.
Wameitaka serikali iangalie barabara
hiyo inayounganisha mikoa ya Simiyu, Shinyanga pamoja na Arusha.
Baadhi ya wakazi wa vijiji vya jirani na eneo hilo wamesema mafuriko
hayo yamesimamisha huduma zote za kijamii katika eneo hilo kwa kuwa
daraja lililojaa maji ndiyo kiungo muhimu cha kufika eneo yenye huduma.
Wamesema kwamba serikali mara kadhaa imeahidi kuliboresha bila matumani huku
ikijuwa dawa pekee ya sehemu hiyo ni kujenga daraja refu na mwenyekiti
wa kitongoji cha maokoni mkuya nyinyi akidai hata wagonjwa wameshindwa
kwenda hospitalini.
Via>>ITV
Social Plugin