Timu ya Yanga ya Tanzania imefanikiwa kuitupa nje ya mashindano timu ya
Platinum FC ya nchini Zimbabwe baada ya mchezo wa marudiano uliopigwa
leo nchini Zimbabwe katika uwanja wa Mandava kumalizika kwa Platinum kupata ushindi wa bao 1-0.
Ushindi iliyopata Platinum umeshindwa kuivusha timu hiyo, kwani katika
mchezo wa kwanza Yanga iliichapa mabao 5-1 katika dimba la taifa jijini
Dar es salaam, hivyo Yanga imevuka kuingia hatua ya 16 bora ya michuano hiyo kwa ushindi wa jumla ya mabao 5-2.
Labda matokeo ya mechi ya kwanza ambayo ilichezwa Tanzani kati ya timu hiyo na Yanga ambayo iliibuka na ushindi wa goli 5-1 iliwafanya mabingwa hao kucheza mchezo huu kwa ujasiri mkubwa sana, huku wenzao wakijiongeza nguvu ya ziada ili wapate matokeo mazuri nyumbani kwao.
Dakika 90 zilikamilika zikaongezwa nyingine nne lakini haikusaidia kubadili matokeo hayo, FC Platinum walitoka na ushindi wa goli 1-0, lakini matokeo hayo bado yanaipa nafasi Yanga kuendelea na mashindano hayo huku safari ya Platinum ikiishia hapohapo nyumbani kwao kwenye Uwanja wa Mandava.
Katika hatua ya 16 Bora Yanga inasubiri kukutana na timu moja wapo kati
ya Benfica de Luanda ya Angola au Étoile Sportive du Sahel ya Tunisia
ambazo zinarudiana kesho nchini Angola.
Katika mchezo wa kwanza Étoile Sportive du Sahel ilishinda kwa bao 1-0 katika mchezo uliopigwa nchini Tunisia.
Social Plugin