ANGALIA PICHA- ASILIMIA 50 YA BARABARA ZA MANISPAA YA SHINYANGA ZIMEOZA!!
Thursday, May 07, 2015
Meya wa manispaa ya Shinyanga Gulam Hafeez Mukadam akishangaa shimo kubwa katika moja ya barabara ya kata ya Kitangiri(Sokoine Road)
Leo
na meya wa manispaa ya Shinyanga Gulam Hafeez Mukadam (kushoto)ameanza ziara ya kutembelea barabara za kata za manispaa hiyo kujionea
hali halisi ya miundombinu ya barabara
katika manispaa hiyo ambapo ametembelea kata 8 kati ya 17 ambazo ni Kolandoto,Ibadakuli Kitangiri,Ndala,Kambarage,Mwawaza,Masekelo,Ngokolo na
Mhandisi wa barabara katika halmashauri ya manispaa ya Shinyanga George Medard aliyekuwa ameambatana na meya wa manispaa ya Shinyanga Gukam Hafeez Mukadam akiwa katika barabara ya Kolandoto -Galamba katika kata ya Kolandoto wakati wa ziara ya kutembelea barabara za kata za manispaa hiyo kujionea hali halisi ya miundombinu ya barabara katika manispaa hiyo ikiwa ni maazimio ya kikao kilichopita cha baraza la madiwani wa manispaa hiyo.Medard alisema changamoto inayowakabili ni ufinyu wa bajeti
Hapa ni Katika kata ya Ibadakuli-Katikati ni diwani wa kata hiyo Leonard Mayunga akimwonesha meya huyo jinsi barabara ya Ugweto-Ipeja ilivyo korofi hivyo kuhitaji msaada wa haraka ili barabara hiyo pamoja na ile ya Ibadakuli-Uzogore zitengenezwe ili kuwaondolea kero wananchi
Hii ni barabara ya Ugweto-Ipeja miongoni mwa barabara mbovu katika manispaa ya Shinyanga ambapo meya wa manispaa ya Shinyanga Gulam Hafeez Mukadam anasema asilimia
50 ya barabara zote za halmashauri ya manispaa ya Shinyanga zimeharibika
kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha hali inayosababisha usumbufu kwa
watumiaji wa barabara hizo.
Diwani wa kata ya Ibadakuli Leonard Mayunga akimsisitiza meya juu ya umuhimu wa kutengeneza barabara akiomba zitengwe fedha za dharura kunusuru barabara za manispaa hiyo
Hapa ni katika kata ya Kitangiri-Katikati ni diwani wa kata hiyo George Kitalama akionesha moja ya barabara katika kata hiyo inayoendelea kujengwa ingawa barabara nyingi katika kata hiyo kubwa ni mbovu na nyingi hazipitiki kutokana na mashimo na zingine kukatwa na maji ya mvua
Meya wa manispaa ya Shinyanga Gulam Hafeez Mukadam akishangaa shimo kubwa katika moja ya barabara ya kata ya Kitangiri(Sokoine Road)
Diwani wa kata ya Kitangiri George Kitalama akionesha barabara zake mbovu
Hapa ni katika barabara inayotenganisha kata ya Ndala na Masekelo lakini pia inakwenda hadi kata ya Masekelo,barabara ambayo ni korofi pia,imebomolewa na maji ya mvua huku mashimo ya kila aina yakitawala
Meya wa manispaa hiyo amesema kutokana na bajeti kuisha hivi sasa wanajipanga
namna ya kusaidia miundombinu hiyo irudi katika hali ya kawaida ingawa hali
katika baadhi ya barabara inaridhisha.
Barabara hiyo ikiwa imemomonyoka
Meya akijadili jambo na mhandisi wake
Barabara kuelekea kata ya Mwawaza karibu na panapojengwa hospitali ya rufaa ya mkoa wa Shinyanga
Hapa ni katika daraja la Mto Ndama-daraja ambalo limejengwa na mkandarasi Mega Teck wa Tanga,hii sehemu inaelezwa kuwa ilikuwa korofi hivyo manispaa ya Shinyanga imeondoa changamoto hiyo sasa wananchi wanapita kwa raha kama unavyoona pichani
Muonekano wa daraja hilo
Mhandisi wa barabara katika halmashauri ya manispaa ya Shinyanga George Medard akiangalia daraja la mto Ndama
Hapa ni katika kata ya Kambarage- Katika barabara ya Kambarage-Ndala,barabara ikiwa imeharibika vibaya
Hapa ni katika kata ya Ngokolo-Meya akiwa katika shimo kubwa karibu na Hotel nyingi za eneo hilo karibu na ofisi ya afisa mtendaji wa kata hiyo
Ndiyo muonekano wa barabara za manispaa ya Shinyanga
Meya wa manispaa ya Shinyanga Gulam Hafeez Mukadam akizungumza katika kata ya Ngokolo ambapo amesema kabla ya mvua barabara nyingi zilikuwa nzuri na
zenye kiwango na baada kuanza sura nzima ya manispaa ikabadilika kutokana na
barabara kukatika na kuwepo kwa mashimo mengi barabarani.
Aliongeza kuwa kutokana na bajeti kuisha hivi sasa wanajipanga
namna ya kusaidia miundombinu hiyo irudi katika hali ya kawaida ingawa hali
katika baadhi ya barabara inaridhisha.
Gulam alisema tayari ameshazungumza na injinia wa manispaa
ya Shinyanga na sasa wanatafuta mafuta kwa ajili ya kutumia greda la manispaa
hiyo na kwamba wanafanya jitihada za kuomba pesa za dharura kutoka bodi ya
barabara ili ziwasaidie kujenga barabara hizo.Alisema barabara zingine zitajengwa kwa mradi wa benki ya dunia.
Picha zote na Kadama Malunde-Malunde1 blog
Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com
Social Plugin