AJALI YA BAJAJI NA LORI YAUA MWENDESHA BAJAJI HUKO NZEGA
Tuesday, May 05, 2015
Ajali za barabarani zimeendelea kupoteza maisha ya Watanzania ambapo leo asubuhi Mwendesha bajaji aliyejulikana kwa jina la Hussein Masha mkazi wa Nzega Ndogo wilayani Nzega mkoani Tabora amefariki dunia baada ya kugongwa na gari aina ya Tipa.
Mashuhuda wa ajali hiyo wameiambia Malunde1 blog kuwa mwendesha bajaji huyo alikuwa anatoka Nzega Ndogo kuelekea Nzega
mjini ,alipofika katika eneo la Kitongo akataka kukata kona kuingia barabara ya
posta ndipo tipa lililokuwa nyuma yake likagonga na kusababisha kifo chake papo
hapo huku mwenye tipa akikimbia
Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com
Social Plugin