Rais
wa jamhuri ya Msumbiji Filipe Nyussi amesema vita dhidi ya ugaidi na
ufisadi ni vita ambayo inatakiwa kupigana kwa pamoja hivyo uhusiano
mzuri uliopo kati ya Tanzania na nchi yake ukitumika vyema utaweza
kumudu vita hiyo.
Mh Nyussi ametoa rai hiyo bungeni mjini Dodoma alipokuwa anahutubia
wabunge ambapo amesema ili kupambana na umaskini katika nchi hizi mbili
jambo kubwa ni kufanya kazi kwa pamoja na kila mmoja kumuheshimu
mwenzake, ambapo kabla ya hotuba hiyo ametembelea makao makuu ya chama
cha mapinduzi.
Kwa upande wake spika wa bunge Mh Anne Makinda amemweleza rais
Nyussi kuwa bunge lake liko bega kwa bega na serikali yake na kwamba
wataendeleza ushirikiano uliopo kwa manufaa ya nchi zote mbili.
Mara baada ya hotuba yake bunge limeendelea utaratibu wake ambapo
waziri wa nchi muungano Mh Samia Suluhu Hassan amewasilisha bungeni
makadirio ya mapato na matumizi ya ofisi ya makamu wa rais kwa mwaka huu
wa fedha na kueleza mafanikio yaliyopatikana katika awamu ya nne pamoja
na namna ambavyo changamoto zilizopo zinavyoshughulikiwa.
Akisoma maoni ya kambi rasmi ya upinzani upande wa ofisi ya makamu
wa rais muungano Mh Tundu Lissu yamedai kuwa maagizo ya kambi hiyo
yaliyotolewa mwaka jana yamepuuzwa ambayo ni pamoja na utoaji wa taarifa
kuhusu fedha zote zinazopelekwa Zanzibar kupitia hazina au mamlaka
yoyote ziwasilishwe ofisi ya makamu wa rais muungano huku kamati nazo
zikiwasilisha taarifa zake na kuitaka serikali kubomoa nyumba zote
zilizojengwa kinyume na sheria katika fukwe za bahari na kingo za mito.
Via>>ITV
Social Plugin