Mahakama ya wilaya ya Bariadi mkoani Simiyu,
imemhukumu Ahmed Ismael (34) mfanyabiashara mkazi wa Salunda Bariadi mjini
kwenda jela mwaka mmoja au kulipa faini shilingi 2000 kwa kosa la kupatikana na hatia ya
kutumia silaha kwenye mkusanyiko wa watu.
Mahakama hiyo ilitoa adhabu kwa mshitakiwa huyo,
ambaye ni kada wa Chama Cha Mapinduzi wilayani Bariadi, chini ya sheria ya makosa
ya jinai kifungu namba 4(1),(2) na (8) cha sheria za mikusanyiko ( Public Order
Act) sura namba 385 kama ilivyofanyiwa marekebisho mwaka 2012.
Akisomewa makosa yanayomkabili na mwendesha
mashtaka mwanasheria wa serikali Mkoani Simiyu Yamiko Mlekano, alisema mtuhumiwa anatuhumiwa wa makosa mawili.
Yamiko alisema kosa la kwanza mnamo tarehe
22/04/2015 majira ya saa 10-12 jioni mshitakiwa akiwa katika mkusanyiko wa watu
ndani ya kijiji cha Isanga wilaya ya Bariadi alipatikana na silaha aina ya
Pistol (TISAS) yenye namba za usajili No.0620-11J00502.
Alibainisha kosa la pili kuwa siku na tarehe hizo
hizo mshitakiwa akiwa katika maeneo ya Salunda kando kando ya Barabara kuu ya
Bariadi-Maswa katika mkusanyiko wa watu alipatikana na kutumia silaha hiyo
kinyume cha sheria.
Mbele ya hakimu mkazi mwandamizi wa mahakama hizo
Aidan Mwilapwa, mshtakiwa alikiri makosa yote, huku mwendesha mashtaka huyo
akiitaka mahakama kutoa adhabu kali kwa mtuhumiwa hiyo ili iwe fundisho kwa
watu wengine.
Akitoa hukumu juu ya makosa hayo hakimu Mwilapwa
alisema kosa la kwanza mahakama imetoa adhabu ya kifungo cha kwenda jela
miazi 6 au kulipa faini shilingi 1000, na kosa la pili kifungo jela miezi 6 au
faini shilingi 1000.
Kwa makosa yote mahakama ilimuhukumu kwenda jela
mshitakiwa kifungo cha kwenda jela mwaka 1 au faini shilingi 2000, ambapo
aliweza kulipa faini hiyo na kuanikiwa kuwa huru.
Hivi
karibu wakati Mbunge
wa Bariadi Magharibi Andrew (CCM) Chenge alinusurika kipigo kutoka kwa wafuasi
wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) mkoani Simiyu baada ya kupita
katika ofisi zao akitoka kwenye mkutano wake.
Wakati akipita katika ofisi za chama
hicho wafuasi waliokuwepo walianza kuushambulia kwa mawe msafara wa mbunge huyo
kwa kile kilichoelezwa kuwa alikuwa akiwapigia kelele kutokana na moja ya gari
lake la matangazo likiwa linapiga muziki wa chama chake (CCM).
Kutokana na tafrani hiyo Mfuasi huyo
ambaye ni kada mkubwa wa CCM wilayani Bariadi, alirusha risasi 2 hewani kwa lengo
la kuwatawanya wafuasi wa chadema walikuwa wakirusha mawe, huku akieleza kuwa
sababu ya kurusha risasi ni kutaka kumuokoa mbunge huyo asipigwe na wafuasi
hao.
Social Plugin