ANGALIA PICHA- KIKAO CHA WAANDISHI WA HABARI NA TAWLAE LEO MJINI SHINYANGA

Hapa ni katika Ukumbi wa Mwalimu House mjini Shinyanga ambapo leo kumefanyika kikao cha Waandishi wa Habari kilichoandaliwa na Chama Cha Viongozi Wanawake Wataalam wa Kilimo na Mazingira (Tanzania Association Of Women  Leadership in Agriculture and  Environment-TAWLAE),mgeni rasmi alikuwa afisa Maendeleo ya Jamii na Vijana katika halmashauri ya wilaya ya Shinyanga Daudi Kisangure.
Awali Katibu wa Chama Cha Viongozi Wanawake Wataalam wa Kilimo na Mazingira (Tanzania Association Of Women  Leadership in Agriculture and  Environment-TAWLAE),Hellen Maleza akieleza lengo la kikao hicho ambapo alisema
ni kushawishi waandishi wa habari na kuhamasisha kutoa elimu kwa jamii na watunga sera kuhusu umuhimu wa wazee katika jamii.
Alisema lengo jingine ni kubainisha kuhusu utekelezaji wa masuala ya wazee mkoani Shinyanga pamoja na changamoto zilizopo sambamba na kuweka mikakati na kuongeza nguvu za pamoja za kusemea masuala ya wazee na kutoa msukumo kwa watunga sera. .


Mwandishi wa habari Greyson Kakuru akizungumza katika kikao hicho kilicholenga kujadili mambo yanayohusu wazee.
Mzee kwa mujibu wa Sera ya Taifa ya Wazee ni wenye umri wa kuanzia miaka Miaka 60 na kwa  Mujibu wa Sensa ya Watu na Makazi - 2012, Wazee Miaka 60 na kuendelea ni asilimia 5.6 (2,507,568 Kati yao 1,307,358 ni Wanawake na 1,200,210 Wanaume.
Waandishi wa habari wakiwa ukumbini-
Mikoa ya Kilimanjaro, Pwani, Lindi na Mtwara, inaonyesha idadi kubwa ya wazee ikiwa na asilimia 7,  6.7,  6.3 na 6.2 kama inavyo fuatana.

Kushoto ni
Mratibu wa Chama Cha Viongozi Wanawake Wataalam wa Kilimo na Mazingira (Tanzania Association Of Women  Leadership in Agriculture and  Environment-TAWLAE), Eliasenya Nnko ,katikati mgeni rasmi Afisa Maendeleo ya Jamii na Vijana katika halmashauri ya wilaya ya Shinyanga Daudi Kisangure,kulia ni mwandishi wa habari Sam Bahari aliyekuwa mwenyekiti wa kikao hicho

Mratibu wa Chama Cha Viongozi Wanawake Wataalam wa Kilimo na Mazingira (Tanzania Association Of Women  Leadership in Agriculture and  Environment-TAWLAE), Eliasenya Nnko akizungumza katika kikao hicho ambapo alisema 80% ya wazee wanaishi Vijijini na 50% ya yatima wote Tanzania wanatunzwa na wazee, Mara nyingi ni wazee Wanawake.
Kikao kinaendelea
Mratibu wa TAWLAE, Eliasenya Nnko alisema
Wazee 2,866 waliuawa kwa imani za ushirikina katika Mikoa 10 kwa kipindi cha Miaka 5, - wastani wa mauaji 573 kila Mwaka  na Karibu asilimia 60% ya Vifo vyote miongoni mwa wazee wa umri wa Miaka  60 na kuendelea katika baadhi ya Wilaya Nchini vinasababishwa na Magonjwa yasiyo ya kuambukizwa (NCDs).

Mwenyekiti wa kikao hicho Sam Bahari akimkaribisha mgeni rasmi

Mgeni rasmi Afisa Maendeleo ya Jamii na Vijana katika halmashauri ya wilaya ya Shinyanga Daudi Kisangure  akifungua kikao hicho
Mhasibu wa TAWLAE Adelina Chongolo akiandika dondoo muhimu za kikao hicho.
Afisa Maendeleo ya Jamii na Vijana katika halmashauri ya wilaya ya Shinyanga Daudi Kisangure  alisema wazee ni hazina kubwa hivyo wanapaswa kuthaminiwa kwa kupatiwa huduma zote muhimu

Mratibu wa TAWLAE), Eliasenya Nnko akiwasilisha taarifa ya mradi wa Uwajibikaji(Accountability Project) unaotekelezwa mkoani Shinyanga
Maelezo kuhusu mradi huo

 Mwandishi wa habari Kadama Malunde akifuatilia kilichokuwa kinajiri ukumbini
Afisa Maendeleo ya Jamii na Vijana katika halmashauri ya wilaya ya Shinyanga Daudi Kisangure akitoa taarifa juu ya utekelezaji wa masuala ya wazee katika wilaya yake.

Kikao kinaendelea

Mganga mkuu wa wilaya ya Shinyanga Dkt Emmanuel Kadelya Joha  akiwasilisha taarifa ya utoaji wa huduma ya afya kwa wazee ambapo alisema ili kumaliza tatizo la changamoto ya huduma za afya kwa wazee tayari jumla ya wazee 3000 kati ya 11,000 wamepigwa picha na watapatiwa vitambulisho katika awamu ya kwanza.

Mganga mkuu wa wilaya ya Shinyanga Dkt Emmanuel Kadelya Joha  akionesha mfano wa vitambulisho kwa ajili ya wazee ambapo alisema zoezi la kuwapatia wazee vitambulisho kwa ajili ya matibabu ni endelevu na wazee wanaendelea kujaza fomu katika ofisi za vijiji na kata ili kuhakikisha kuwa hawapati usumbufu wanapofika katika vituo vya afya na hospitali.

Mwandishi wa Habari Veronica Natalis akichangia mawili matatu katika kikao hicho

Mwandishi wa habari Stephen Wang’anyi akichangia kilichokuwa kinaendelea ukumbini

Mwenyekiti wa Baraza la Wazee wilaya ya Shinyanga Vijijini Edward Lupimo akizungumza katika kikao hicho ambapo alihimiza waandishi wa habari kutumia kalamu zao katika kuandika masuala yanayowahusu wazee kwani vijana wa leo ndiyo wazee wa kesho.

Mikakati iliyofikiwa katika kikao hicho kuhusu wazee nchini

Waandishi wa habari Suzy Butondo na Stephen Kidoyayi wakifuatilia kilichokuwa kinaendelea

Miongoni mwa changamoto zilizobainishwa katika kikao hicho zinazowakabili kuhusu huduma ya afya kwa wazee ni pamoja na Watumishi wa Afya kutoelewa vizuri mahitaji ya Kiafya ya wazee (Geriatric Care) ,Upungufu wa Madawa na huduma nyinginezo katika Vituo vya Afya/Hospitali za Serikali ,Tatizo la upatikananji wa Dawa/Matibabu ya Magonjwa yanayowasibu wazee (NCDs), Kisukari, Moyo, Miguu, Macho n.k

Changamoto zingine ni Lugha zisizo rafiki kwa wazee,Wazee wanakataliwa huduma bila malipo,Ukosefu wa pato kulipia gharama za usafiri kwenda Hospitali/kununua Dawa,Matibabu bila malipo kuwa kwenye Hospitali za Serikali tu (Zaidi ya 40% ya Tiba nchini zinatolewa na vituo vya watu binafsi na Maagizo ya Serikali kwa kila Halmashauri kuwa na Kitengo na Mratibu wa Afya wa wazee kutotekelezwa.

Baadhi ya vikwazo vinavyosababisha wazee kutopatiwa haki za ni pamoja na Mtizamo hasi wa Jamii Kwa wazee,Sera na matamko kuhusu wazee kutotungiwa Sheria,Upungufu wa takwimu zinazohusu wazee,Kukosa uwakilishi katika vyombo vya maamuzi (WDC, Full Council, Bunge),Baadhi ya wenye mamlaka kutopenda kuwapatia wazee hata yale yaliyo kwenye Sera na miongozo ya taifa mfano-Mikopo Kina mama na Kutoanzishwa/kuimarishwa kwa mabaraza huru ya wazee kuwapa sauti.

Picha zote na Kadama Malunde-Malunde1 blog

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com
Previous Post Next Post