ANGALIA PICHA- KINGINE KIKUBWA KUTOKA WILAYA YA SHINYANGA LEO

Hili ni jengo jipya la ofisi ya mkuu wa wilaya ya Shinyanga lililopo mjini Shinyanga.Leo Mei 14,2015 mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro amekutana na waandishi wa habari waliopo katika wilaya hiyo na kujadili mambo mbalimbali kuhusu maendeleo ya wilaya hiyo.Kabla ya kikao na waandishi wa habari mkuu huyo wa wilaya aliongoza zoezi la kupanda miti nje ya jengo hilo jipya ambapo waandishi wa habari na  wafanyakazi wa ofisi ya wilaya hiyo kila mmoja alipanda mti mmoja


Kushoto ni mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akizungumza wakati wa zoezi la kupanda miti nje ya jengo la ofisi ya mkuu wa wilaya.Alisema wameamua kupanda miti ili kupendezesha ofisi hiyo mpya lakini pia ikiwa ni njia ya kuhamasisha wananchi kupanda miti katika mazingira yao huku akisisitiza kuwa miti inayotakiwa kupandwa kuwa ni ile ya matunda,kivuli lakini pia kwa ajili ya mbao
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akipanda mti
Wafanyakazi wa wilaya ya Shinyanga na waandishi wa habari wakishuhudia mkuu wa wilaya ya Shinyanga akipanda mti
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga akimwagilia maji mti alioupanda
Afisa afya mkuu wa manispaa ya Shinyanga Elly Nakuzelwa akipanda mti kwa niaba ya mkurugenzi wa manispaa ya Shinyanga

Makamu mwenyekiti wa kamati ya maadili Klabu ya Waandishi wa habari mkoa wa Shinyanga Sam Bahari akipanda mti


Katibu tawala wilaya ya Shinyanga Boniphace Chambi akipanda mti

Wafanyakazi wa ofisi ya wilaya ya Shinyanga wakimwagilia maji mti 

Zoezi la kupanda miti linaendelea

Katibu wa Klabu ya waandishi wa habari mkoa wa Shinyanga Kareny Masasy akipanda mti

Mhariri wa Habari kutoka Radio Faraja bi Moshi Ndugulile akipanda mti

Wafanyakazi wa ofisi ya wilaya ya Shinyanga na waandishi wa habari wakipanda miti

Mkurugenzi wa Malunde1 blog,bwana Kadama Malunde akipanda mti nje ya jengo la ofisi ya mkuu wa wilaya ya Shinyanga

Wafanyakazi wa ofisi ya mkuu wa wilaya ya Shinyanga baada kumaliza kupanda miti

Kushoto ni mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akitoa maelekezo baada ya kumaliza kupanda miti nje ya ofisi ya mkuu wa wilaya hiyo leo

Hapa ni ndani ya ofisi ya mkuu wa wilaya-Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akizungumza na waandishi wa habari ambapo alihamasisha wananchi kushiriki katika shughuli mbalimbali za maendeleo huku akiwataka kuisoma vizuri katiba inayopendekezwa ili waielewe na muda utakapofika wapigie kura katiba badala ya kufuata maneno ya wanasiasa  majukwaani.Hali kadhalika akawaomba wananchi kujitokeza kujiandikisha kwenye daftari la wapiga kura muda utakapofika


 Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro pia alikemea vitendo vya mauaji ya watu wenye ulemavu wa ngozi(albino) na vikongwe huku akiitaka jamii kushirikiana kwa pamoja kuimalisha ulinzi katika maeneo yao na kusisitiza kuwa maendeleo ya watanzania yataletwa na watanzania wenyewe

Mwandishi wa habari gazeti la Jamboleo Stephen Kidoyayi akiuliza swali katika ofisi ya mkuu wa wilaya

Mkuu wa wilaya Josephine Matiro akisikiliza kwa umakini zaidi maswali na michango mbalimbali ya waandishi wa habari

Mwandishi wa habari gazeti la Majira Abeid Suleiman akizungumza katika ofisi ya mkuu wa wilaya

Mkuu wa wilaya akizungumza na waandishi wa habari

Waandishi wa habari wakiwa katika ofisi ya mkuu wa wilaya ya Shinyanga leo

Katibu tawala wilaya ya Shinyanga Boniphace Chambi akisisitiza jambo wakati wa kikao hicho

Afisa afya mkuu wa manispaa ya Shinyanga Elly Nakuzelwa akizungumza katika kikao hicho

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com
Previous Post Next Post