|
Hapa ni kwenye Lango kuu la Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Shinyanga ambako leo kulifanyika maandamano ya w
auguzi kutoka mkoa huo kuanzia hospitalini hapo hadi kwenye Viwanja vya Shycom mjini Shinyanga ambako leo kumefanyika uzinduzi wa Siku ya Wauguzi duniani ambayo hufanyika Mei 12,kila mwaka.Mgeni rasmi katika uzinduzi huo alikuwa mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro kwa niaba ya mkuu wa mkoa wa Shinyanga Ally Nassoro Rufunga.
Maadhimisho ya siku ya Wauguzi Duniani mwaka huu yanafanyika kitaifa mkoani Shinyanga na kilele chake kitakuwa kesho Jumanne,Mei 12,2015.
Kauli mbiu ya Siku ya Uuguzi duniani mwaka huu ni "Wauguzi ni kiini cha mabadiliko,huduma bora kwa gharama nafuu".
Mwandishi wa Malunde1 blog,Kadama Malunde alikuwepo kwenye tukio hilo ametuletea picha nyingi tu Angalia hapa chini |
|
Wauguzi wakiwa katika maandamano hayo |
|
Wanafunzi kutoka Chuo cha Uuguzi Kolandoto wakiwa katika maandamano hayo kuelekea viwanja vya Shycom mjini Shinyanga ambako ndiko maadhimisho hayo yanafanyika |
|
Usalama barabarani ulikuwepo wa kutosha |
|
Waandamanaji wakipita karibu na ofisi za TANESCO mjini Shinyanga |
|
Wapiga tarumbeta wakifanya yao |
|
Wauguzi wakiandamana |
|
Maandamano yanaendelea |
|
Mgeni rasmi Mkuu wa wilaya ya Shinyanga kwa niaba ya mkuu wa mkoa wa Shinyanga bi Josephine Matiro akiwasili katika viwanja vya Shycom mjini Shinyanga na kusalimiana na baadhi ya viongozi wa mkoa wa Shinyanga |
|
Mgeni rasmi Mkuu wa wilaya ya Shinyanga kwa niaba ya mkuu wa mkoa bi Josephine Matiro akikagua moja ya mabanda yanayotoa huduma mbalimbali za afya kama vile kupima afya,kutoa damu,tohara na ushauri mbalimbali wa kiafya |
|
Hapa ni katika banda la vyuo vya uuguzi ambao wanafanya maonesho ya taaluma ya uuguzi |
|
Muuguzi akionesha kwa vitendo namna akina mama wanavyojifungua |
|
Ndani ya moja ya mabanda |
|
Mtaalam kutoka Red cross akitoa maelekezo kwa mgeni rasmi katika banda lao la kutolea damu |
|
Waandamanaji wakiwasili katika viwanja vya Shycom |
|
Meza kuu wakiwa wamesimama kupokea maandamano |
|
MC akifanya yake wakati wa kupokea maandamano |
|
Aliyesimama ni muuguzi mkuu wa mkoa wa Shinyanga Dkt Fabian Kalabwe akikaribisha wageni |
|
Meza kuu wakifuatilia kinachojiri |
|
Wanakwaya kutoka chuo cha Uuguzi Kolandoto wakitoa burudani |
|
Wageni mbalimbali wakifuatilia kilichokuwa kinajiri |
|
Mganga mkuu wa mkoa wa Shinyanga Dkt Ntuli Kapologwe akizungumza wakati wa ufunguzi maadhimisho ya siku ya Wauguzi kitaifa yanayofanyika mkoani Shinyanga |
|
Wauguzi wakiwa eneo la tukio |
|
Muuguzi mkuu wa mkoa wa Shinyanga Dkt Fabian Kalabwe akisoma risala |
|
Wanenguaji kutoka kundi la Medical Culture wakitoa burudani |
Bendi ya Medical Culture wakitoa burudani
|
Mnenguaji matata kutoka kundi la Medical Culture akionesha mbwembwe zake.
Kaimu muuguzi mkuu wa serikali Dkt Ama Kasangala akitoa salamu za serikali na kuzungumzia maana ya siku ya Wauguzi Duniani ambayo hulenga kukumbushana mambo mbalimbali waliyofanya wauguzi na kupanga mikakati mbalimbali ya namna ya kutoa huduma kwa wananchi.Dkt Kasangala aliwataka wauguzi nchini kutoa huduma za afya kwa wananchi wakati serikali inaboresha mazingira yao ya kazi |
|
Mgeni rasmi mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro kwa niaba ya mkuu wa mkoa wa Shinyanga akizungumza wakati akizindua Siku ya Uuguzi duniani ambayo hufanyika Mei 12,kila mwaka.Matiro alisema upo umuhimu kwa wanaume kushiriki katika suala la uzazi wa mpango na wakati mwingine washuhudie jinsi akina mama wanavyojifungua ili wawaheshimu akina mama. |
|
Mkuu huyo wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro alizungumzia pia umuhimu wa wananchi kutumia vyandarua vyenye viwatilifu |
|
Picha ya pamoja baada ya uzinduzi |
|
Picha ya pamoja baada ya uzinduzi |
Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com