Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

ANGALIA PICHA- UZINDUZI MAADHIMISHO YA SIKU YA UUGUZI DUNIANI YANAYOFANYIKA KITAIFA MKOANI SHINYANGA

Hapa ni kwenye Lango kuu la Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Shinyanga ambako leo kulifanyika maandamano ya w
auguzi kutoka mkoa huo kuanzia hospitalini hapo hadi kwenye Viwanja vya Shycom mjini Shinyanga ambako leo kumefanyika uzinduzi wa Siku ya Wauguzi duniani ambayo hufanyika Mei 12,kila mwaka.Mgeni rasmi katika uzinduzi huo alikuwa mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro kwa niaba ya mkuu wa mkoa wa Shinyanga Ally Nassoro Rufunga.

Maadhimisho ya siku ya Wauguzi Duniani mwaka huu yanafanyika kitaifa mkoani Shinyanga na kilele chake kitakuwa kesho Jumanne,Mei 12,2015.

Kauli mbiu ya
Siku ya Uuguzi duniani  mwaka huu ni "Wauguzi ni kiini cha mabadiliko,huduma bora  kwa gharama nafuu".

Mwandishi wa Malunde1 blog,Kadama Malunde alikuwepo kwenye tukio hilo ametuletea picha nyingi tu Angalia hapa chini

Wauguzi wakiwa katika maandamano hayo

Wanafunzi kutoka Chuo cha Uuguzi Kolandoto wakiwa katika maandamano hayo kuelekea viwanja vya Shycom mjini Shinyanga ambako ndiko maadhimisho hayo yanafanyika

Usalama barabarani ulikuwepo wa kutosha

Waandamanaji wakipita karibu na ofisi za TANESCO mjini Shinyanga

Wapiga tarumbeta wakifanya yao

Wauguzi wakiandamana

Maandamano yanaendelea

Mgeni rasmi Mkuu wa wilaya ya Shinyanga kwa niaba ya mkuu wa mkoa wa Shinyanga bi Josephine Matiro akiwasili katika viwanja vya Shycom mjini Shinyanga na kusalimiana na baadhi ya viongozi wa mkoa wa Shinyanga

Mgeni rasmi Mkuu wa wilaya ya Shinyanga kwa niaba ya mkuu wa mkoa bi Josephine Matiro akikagua moja ya mabanda yanayotoa huduma mbalimbali za afya kama vile kupima afya,kutoa damu,tohara na ushauri mbalimbali wa kiafya
Hapa ni katika banda la vyuo vya uuguzi ambao wanafanya maonesho ya taaluma ya uuguzi 

Muuguzi akionesha  kwa vitendo namna akina mama wanavyojifungua

Ndani ya moja ya mabanda 

Mtaalam kutoka Red cross akitoa maelekezo kwa mgeni rasmi katika banda lao la kutolea damu

Waandamanaji wakiwasili katika viwanja vya Shycom

Meza kuu wakiwa wamesimama kupokea maandamano

MC akifanya yake wakati wa kupokea maandamano

Aliyesimama ni muuguzi mkuu wa mkoa wa Shinyanga Dkt Fabian Kalabwe akikaribisha wageni

Meza kuu wakifuatilia kinachojiri 

Wanakwaya kutoka chuo cha Uuguzi Kolandoto wakitoa burudani

Wageni mbalimbali wakifuatilia kilichokuwa kinajiri

Mganga mkuu wa mkoa wa Shinyanga Dkt Ntuli Kapologwe akizungumza wakati wa ufunguzi  maadhimisho ya siku ya Wauguzi kitaifa yanayofanyika mkoani Shinyanga

Wauguzi wakiwa eneo la tukio

Muuguzi mkuu wa mkoa wa Shinyanga Dkt Fabian Kalabwe akisoma risala 

Wanenguaji kutoka kundi la Medical Culture wakitoa burudani

                        Bendi ya  Medical Culture wakitoa burudani

Mnenguaji matata kutoka kundi la Medical Culture  akionesha mbwembwe zake.
 
Kaimu muuguzi mkuu wa serikali Dkt  Ama Kasangala akitoa salamu za serikali na kuzungumzia maana ya siku ya Wauguzi Duniani ambayo hulenga kukumbushana mambo mbalimbali waliyofanya wauguzi na kupanga mikakati mbalimbali ya namna ya kutoa huduma kwa wananchi.Dkt Kasangala aliwataka wauguzi nchini kutoa huduma za afya kwa wananchi wakati serikali inaboresha mazingira yao ya kazi

Mgeni rasmi mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro kwa niaba ya mkuu wa mkoa wa Shinyanga akizungumza wakati akizindua Siku ya Uuguzi duniani ambayo hufanyika Mei 12,kila mwaka.Matiro alisema upo umuhimu kwa wanaume kushiriki katika suala la uzazi wa mpango na wakati mwingine washuhudie jinsi akina mama wanavyojifungua ili wawaheshimu akina mama.

Mkuu huyo wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro alizungumzia pia umuhimu wa wananchi kutumia vyandarua vyenye viwatilifu

Picha ya pamoja baada ya uzinduzi

Picha ya pamoja baada ya uzinduzi
Picha zote na Kadama Malunde-Malunde1 blog
 BOFYA HAPA KUANGALIA PICHA KILELE CHA MAADHIMISHO HAYO

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com