ANGALIA PICHA- WAANDISHI WA HABARI SHINYANGA WATOA MSAADA KWA ALBINO BUHANGIJA "SIKU YA UHURU WA VYOMBO VYA HABARI"


Katika kuadhimisha siku ya Uhuru wa Vyombo wa Habari duniani waandishi wa habari mkoa wa Shinyanga wametembelea kituo cha kulelea watoto wenye ulemavu wa ngozi( Albino),wasioona na wasiosikia cha Buhangija katika manispaa ya Shinyanga.Waandishi hao wa habari wametoa msaada wa chakula kama vile maharage kilo 100,unga kilo 250,mifuko ya saruji minne kwa ajili ya kukamilisha ujenzi wa sakafu katika moja ya mabweni katika kituo hicho na pesa kwa ajili ya wajenzi vyote vikiwa na thamani ya shilingi milioni moja.Pichani ni waandishi wa habari kutoka chama cha Waandishi wa habari mkoa wa Shinyanga wakiongozwa na makamu mwenyekiti wa klabu hiyo Greyson Kakuru wakiwasili katika kituo hicho wakiwa wamebeba mabango-Picha zote na Kadama Malunde-Shinyanga

"Mengi sasa njoo Kanda ya Ziwa Ujionee" lilisomeka moja kati ya mabango hayo

Kauli mbiu ya siku ya uhuru wa vyombo vya habari duniani mwaka huu ni “Acha uandishi wa habari ustawi kuelekea uandishi bora,usawa wa kijinsia na usalama katika zama za ki-digitali”.

Waandishi wa habari wakijadili jambo baada ya kuwasili katika kituo cha Buhangija mapema leo

Waandishi wa habari mkoa wa Shinyanga wakiwa katika kituo cha Buhangija 

Waandishi wa habari wakichukua matukio baada ya kupokelewa na mkuu wa kituo cha Buhangija Peter Ajali( mwenye nguo ya kijani- kushoto)

Watoto wakiwa tayari kabisa kuwasikiliza waandishi hao wa habari

Waandishi wa habari wakiwa Buhangija
Msimamizi mkuu wa kituo cha Buhangija Peter Ajali akizungumza ambapo alisema licha ya waandishi hao wa habari kutoa misaada mbalimbali muhimu lakini hakusita kuwapongeza waandishi wa Habari Mkoa wa Shinyanga kwa kazi nzuri wanayofanya kwani wamekuwa msaada mkubwa katika kutetea watoto wenye ulemavu wa ngozi katika kituo cha Buhangija na kusababisha watu mbalimbali wenye mapenzi mema kutoa misaada kwa watoto hao.


Watoto hao wanakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo ya chakula,mabweni,mavazi na vitanda
Mwalimu Peter Ajali akizungumza kituoni hapo

Watoto wakiwa katika eneo la tukio
Mwandishi wa habari ndugu Stephen Kidoyayi kwa niaba ya katibu wa klabu ya waandishi wa habari mkoa wa Shinyanga akitambulisha waandishi wa habari waliofika katika kituo cha Buhangija
Makamu mwenyekiti wa chama cha waandishi wa Habari mkoni Shinyanga (SPC)Greyson Kakuru akizungumza ambapo alisema waandishi wa habari Mkoa wa Shinyanga kama wanajamii wameamua kutumia siku hiyo muhimu kutoa msaada wa vitu mbalimbali kwa  watoto hao vilivyogharimu kiasi cha shilingi milioni moja.Aliyeshikilia kipaza sauti ni ndugu John Mponeja mwandishi wa habari Channel Ten

Mifuko 25 ya unga iliyotolewa na waandishi wa habari mkoa wa Shinyanga kwa ajili ya watoto wenye ulemavu wa ngozi Buhangija

Mwalimu Peter Ajali akishikana mkono na makamu mwenyekiti wa chama cha waandishi wa Habari mkoni Shinyanga (SPC)Greyson Kakuru  

Makamu mwenyekiti wa chama cha waandishi wa Habari mkoni Shinyanga (SPC)Greyson Kakuru akikabidhi mfuko wa unga kwa mkuu wa kituo cha Buhangija Peter Ajali

Makamu mwenyekiti wa chama cha waandishi wa Habari mkoni Shinyanga (SPC)Greyson Kakuru akikabidhi mfuko wa unga na kushikana mkono na mkuu wa kituo cha Buhangija Peter Ajali

Mkuu wa kituo cha Buhangija Peter Ajali(Kulia) akikabidhi mifuko ya unga kwa watoto hao

Mifuko ya unga,maharage(kulia) na saruji iliyotolewa na waandishi wa habari mkoa wa Shinyanga

Mhariri mkuu wa Malunde1 blog ndugu Kadama Malunde akiwa katika kituo cha Buhangija

Ndani ya Bweni-Makamu mwenyekiti wa chama cha waandishi wa Habari mkoni Shinyanga (SPC)Greyson Kakuru akikabidhi akikabidhi shilingi 35,000/= kwa mkuu wa kituo cha Buhangija Peter Ajali kwa ajili ya kukamilisha ujenzi wa sakafu katika moja ya mabweni katika kituo cha Buhangija

Mwandishi wa habari ITV/Radio One ndugu Frank Mshana akitoka katika bweni linaloendelea kujengwa katika kituo cha Buhangija

Mwandishi wa habari Stephen Wang'anyi akichanganya mchanga na saruji nje ya jengo linaloendelea kujengwa kwa ajili ya watoto hao

Ndugu Kadama Malunde,mkurugenzi wa Malunde1 blog akichanganya mchanga na saruji katika kituo hicho

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com
Previous Post Next Post