Sio kitu cha kawaida eti mtu
kujichagulia jeneza ambalo litatumika kwa ajili ya mazishi yake
akifariki.. lakini kuna stori ambazo zimekuwa zikiandikwa kuhusu baadhi
ya watu kujichagulia kabisa, na kuna moja ilitokea Kenya wiki moja
iliyopita ambapo mzee alijinunulia jeneza miaka mitabo iliyopita,
alipofariki walimzika nalo ikawa story kubwa sana.
Kuna wataalamu Uingereza nao wameamua kufanya ubunifu wa aina hii ya majeneza ambayo kwa kuyaangalia yanavutia.
Kampuni ya Halliday Funeral Suppliers Ltd ni wasambazaji wa majeneza tangu mwaka 1979 na sasa wamekuja na staili mpya baada ya kubuni aina mbalimbali za majeneza.
Kampuni hii ina soko kubwa sana la huduma hii, wana wastani wa kuuza majeneza mpaka 300,000 kwa mwaka.
Social Plugin