ANGALIA PICHA UFUNGUZI RASMI WA MAONESHO YA VIWANDA VIDOGO KANDA YA ZIWA YANAYOFANYIKA MJINI SHINYANGA

Hapa ni katika viwanja vya Shycom mjini Shinyanga ambako panafanyika maonesho ya 13 ya Viwanda Vidogo kanda ya ziwa yaliyoandaliwa na Shirika la Viwanda Vidogo nchini(SIDO).Pichani kundi la ngoma ya Kisukuma “ Wanunguli” kutoka kijiji cha Bugimbagu wilaya ya Shinyanga Vijijini wakitoa burudani,siku ya Jumamosi Mei 30,2015-Picha zote na Kadama Malunde-Malunde1 blog

Mgeni rasmi mkuu wa mkoa wa  Shinyanga Ally Nassoro Rufunga kwa niaba ya waziri wa Viwanda na Biashara nchini Abdallah Kigoda akiwasili katika viwanja vya Shycom mjini Shinyanga ambako panafanyika maonesho ya 13 ya Viwanda Vidogo kanda ya ziwa yaliyoandaliwa na Shirika la Viwanda Vidogo nchini(SIDO).

Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Ally Rufunga akisalimiana na Viongozi mbalimbali-Maonesho hayo yamezinduliwa rasmi Mei 30,2015 ingawa maonesho hayo yameanza Mei 28 mwezi huu na Kilele chake kitakuwa Juni 2015 ambapo wajasiriamali mbalimbali kutoka ndani na nje ya nchi wanaonesha bidha zao katika Viwanja vya Shycom mjini Shinyanga.

Katika maonesho hayo jumla ya wajasiriamali 200 kutoka mikoa ya Tanzania bara na Visiwani pamoja na wajasiriamali kutoka nchini Kenya wanashiriki katika maonesho hayo yaliyoandaliwa na uongozi wa SIDO Kanda ya ziwa kwa kushirikiana na ofisi ya mkuu wa mkoa wa Shinyanga

Mgeni rasmi mkuu wa mkoa wa Shinyanga Ally Rufunga kwa niaba ya waziri wa Viwanda na Biashara akikata utepe ishara ya kuzindua rasmi maonesho hayo.Baada ya kukata utepe mgeni rasmi alitembelea mabanda mbalimbali ya wajasiriamali.Kulia kwake ni Mkurugenzi mkuu wa Shirika la Viwanda Vidogo( SIDO) nchini Injinia  Omary Bakari

Meneja wwa SIDO mkoa wa Shinyanga Athanas Moshi akitoa maelezo kwa mheni rasmi kuhusu kazi mbalimbali zinazofanywa na SIDO

Kundi la ngoma ya jadi ya Wanunguli wakitoa burudani katika viwanja vya Shycom mjini Shinyanga

Wanunguli wakitoa burudani

Meneja wa SIDO mkoa wa Shinyanga Athanas Moshi akizungumza wakati wa Ufunguzi wa maonesho hayo

Mstahiki  meya wa manispaa ya Shinyanga Gulam Hafeez Mukadam akizungumza wakati wa ufunguzi wa maonesho hayo

Mgeni rasmi mkuu wa mkoa wa  Shinyanga Ally Nassoro Rufunga kwa niaba ya waziri wa Viwanda na Biashara nchini Abdallah Kigoda akitoa hotuba yake ambapo aliwataka wajasiriamali nchini kufanya kazi zao kiteknojia zaidi na kuhakikisha wanakuwa wabunifu zaidi kwa kubaini nini na kipi kinahitajika lini na wapi wakitumia rasilimali zilizopo katika maeneo yao.
Rufunga alisema ili kuendeleza viwanda nchini wajasiriamali wanatakiwa kuwa wabunifu zaidi ili kuleta ushindani katika soko la bidhaa wanazozalisha kupitia viwanda vyao vidogo. 
Mgeni rasmi Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Ally Rufunga kwa niaba ya waziri wa viwanda na biashara alitumia fursa hiyo kuwataka wananchi wa Shinyanga kutumia maonesho hayo kujifunza mambo mbalimbali yanayofanywa na wajasiriamali kutoka kanda ya ziwa na wajasiriamali kupata muda wa kubalishana uzoefu wa kazi zao.
Mkuu wa mkoa wa Simiyu Erasto Mbwilo akizungumza wakati wa ufunguzi wa maonesho hayo

Mjasiriamali Paulina Nyanzala akisoma risala kwa niaba ya wajasiriamali 200 ambapo alisema miongoni mwa changamoto wanazokabiliana nazo ni pamoja na ukosefu wa dhamana zinazohitajika na kukubalika katika taasisi za fedha kwa ajili ya kupata mikopo na kwamba changamoto nyingine ni uhaba wa vifungashio vya kisasa vinavyokidhi viwango vya ubora na kukabiliana na soko la ushindani.

Mkurugenzi mkuu wa Shirika la Viwanda Vidogo( SIDO) nchini Injinia  Omary Bakari akizungumza wakati wa ufunguzi wa maonesho hayo ya Viwanda vidogo Kanda ya ziwa ambapo aliwataka wajasiriamali nchini kufanya shughuli zao kiteknolojia na kuwa wabunifu zaidi ili kuhakikisha kuwa viwanda vidogo vinainua hali yao kiuchumi.
Picha zote na Kadama Malunde- Malunde1 blog

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com
Previous Post Next Post