Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

ANGALIA PICHA_WANAFUNZI WA CHUO KIKUU CHA USHIRIKA MOSHI WATOA MSAADA KITUO ALBINO BUHANGIJA SHINYANGA!!!!



Wanafunzi wanaosoma katika chuo kikuu cha Ushirika Moshi tawi la Kizumbi Shinyanga (Moshi Cooperative University-MOCU)  wakiongozwa na rais wao Bright Dominic Muro leo wametembelea kituo cha Kulelea watoto wenye ulemavu wa ngozi(albino),wasiosikia na wasioona cha Buhangija Katika manispaa ya Shinyanga.

Wakiwa katika kituo hicho wametoa misaada mbalimbali ikiwemo unga wa sembe kilo 100,maharage kilo 100,unga wa lishe kilo 40,sabuni ,madaftari makubwa,mafuta ya kupikia na yale ya kujipaka,kalamu,nguo na viatu vyote vikiwa na thamani ya zaidi ya shilingi 500,000/=.

Wanafunzi hao pia wameshiriki shughuli mbalimbali ikiwemo kufanya usafi wa mazingira na kufua nguo za watoto wanaolelewa katika kituo hicho cha Buhangija ambacho sasa kinalea watoto zaidi ya 400 wengi wakiwa ni wenye ulemavu wa ngozi wakikabiliwa na changamoto kubwa ya chakula.

Mwandishi mkuu wa Malunde1 blog,ndugu Kadama Malunde alikuwepo eneo la tukio,Katuletea PICHA ZA TUKIO ZIMA

Wanafunzi wa chuo kikuu cha Ushirika Moshi tawi la Kizumbi Shinyanga  wajiandaa kuchoma moto taka zilizopo katika kituo cha Buhangija mjini Shinyanga
Wanafunzi wa chuo kikuu cha Ushirika Moshi tawi la Kizumbi Shinyanga wakifanya usafi katika kituo cha Buhangija,kushoto ni mwalimu mlezi wa watoto wenye ulemavu katika kituo hicho

Wanafunzi wa chuo kikuu cha Ushirika Moshi tawi la Kizumbi Shinyanga wakiendelea kufanya usafi

Katibu wa kamati ya mfuko wa uchangiaji kwa ajili watu wenye ulemavu wa ngozi  kutoka chuo kikuu cha Ushirika Moshi tawi la Kizumbi Shinyanga Emmanuel Patrick akiwa amebeba uchafu katika kituo cha Buhangija

Katibu wa kamati ya mfuko wa uchangiaji kwa ajili watu wenye ulemavu wa ngozi  kutoka chuo kikuu cha Ushirika Moshi tawi la Kizumbi Shinyanga Emmanuel Patrick akizubua mtaro wa maji machafu

Wanafunzi wa chuo kikuu cha Ushirika Moshi tawi la Kizumbi Shinyanga wakichoma moto taka,kushoto ni mwenyekiti wa kamati ya mfuko wa kuchangia  albino katika chuo kikuu cha Ushirika Moshi tawi la Kizumbi Shinyanga (MOCU) Neema Medard Ngaita
Wanafunzi hao wakifua nguo za watoto wa kituo cha Buhangija,katikati ni mwenyekiti wa kamati ya mfuko wa kuchangia  albino katika chuo kikuu cha Ushirika Moshi tawi la Kizumbi Shinyanga (MOCU) Neema Medard Ngaita

Zoezi la kufua nguo linaendelea-Aliyesimama ni Rais wa serikali ya Wanafunzi wanaosoma katika chuo kikuu cha Ushirika Moshi tawi la Kizumbi Shinyanga (MOCU) Bright Dominic Muro 

Mwanafunzi wa MOCU Rehema Yateri akiwa amebeba ndoo ya maji na beseni kwa ajili ya kufua nguo za watoto hao

Wanafunzi wanaosoma katika chuo kikuu cha Ushirika Moshi tawi la Kizumbi Shinyanga (MOCU) wakiendelea na zoezi la kufua nguo

Mwalimu wa elimu Maalumu katika shule ya msingi Buhangija Sasu Nyanga akizungumza kwa niaba ya mkuu wa kituo cha Buhangija ambapo mbali na kuwashukuru wanafunzi hao kwa kujitolea kuwasaidia watoto hao , aliitaka jamii kuendelea kuwasaidia watoto wanaolelewa kituoni hapo ambao sasa wako zaidi ya 400.

 Wanafunzi wanaosoma katika chuo kikuu cha Ushirika Moshi tawi la Kizumbi Shinyanga (Moshi Cooperative University-MOCU) wakiwa katika kituo cha Buhangija kabla ya kukabidhi msaada wao
Mwalimu wa elimu Maalumu katika shule ya msingi Buhangija Sasu Nyanga alisema hivi sasa kutokana na ongezeko la watoto katika kituo hicho kuna changamoto ya chakula ambapo mlo mmoja tu wa watoto hao ni Kilo 45 za maharage,kilo 75-80 za mchele na unga kilo 70.
Wanafunzi wanaosoma katika chuo kikuu cha Ushirika Moshi tawi la Kizumbi Shinyanga (Moshi Cooperative University-MOCU) wakiwa na watoto katika kituo cha Buhangija
Mwalimu wa elimu Maalumu katika shule ya msingi Buhangija Sasu Nyanga alisisitiza umuhimu wa wadau mbalimbali kuendelea kufika katika kituo hico kuwasaidia watoto hao
Rais wa serikali ya Wanafunzi wanaosoma katika chuo kikuu cha Ushirika Moshi tawi la Kizumbi Shinyanga (MOCU) Bright Dominic Muro akizungumza wakati wa kukabidhi msaada wa chakula na mahitaji mengine muhimu,ambapo aliitaka jamii kushirikiana na serikali katika kupiga vita mauaji ya watu wenye ulemavu wa ngozi nchini Tanzania

Rais Muro alisema amani ya taifa siyo tu taifa kuwa huru dhidi ya vita wala mapigano bali ni watu wanaoishi katika taifa hilo kuwa na amani hivyo kuitaka jamii kwa kushirikiana na serikali kupiga vita kwa nguvu zote mauaji ya abino yanayowafanya waishi bila amani katika taifa lao. 

Kulia ni rais wa serikali ya Wanafunzi wanaosoma katika chuo kikuu cha Ushirika Moshi tawi la Kizumbi Shinyanga (MOCU) Bright Dominic Muro  akikabidhi boksi la madaftari kwa Mwalimu wa elimu Maalumu katika shule ya msingi Buhangija Sasu Nyanga kwa niaba ya mkuu wa kituo cha Buhangija 

Rais wa serikali ya Wanafunzi wanaosoma katika chuo kikuu cha Ushirika Moshi tawi la Kizumbi Shinyanga (MOCU) Bright Dominic Muro na Katibu wa kamati ya mfuko wa uchangiaji kwa ajili watu wenye ulemavu wa ngozi  kutoka chuo kikuu cha Ushirika Moshi tawi la Kizumbi Shinyanga Emmanuel Patrick wakikabidhi gunia la maharage

Katibu wa kamati ya mfuko wa uchangiaji kwa ajili watu wenye ulemavu wa ngozi  kutoka chuo kikuu cha Ushirika Moshi tawi la Kizumbi Shinyanga Emmanuel Patrick akikabidhi mafuta ya kujipaka na kalamu kwa ajili ya watoto wanaolelewa katika kituo cha Buhangija

Rais wa serikali ya Wanafunzi wanaosoma katika chuo kikuu cha Ushirika Moshi tawi la Kizumbi Shinyanga (MOCU) Bright Dominic Muro na Katibu wa kamati ya mfuko wa uchangiaji kwa ajili watu wenye ulemavu wa ngozi  kutoka chuo kikuu cha Ushirika Moshi tawi la Kizumbi Shinyanga Emmanuel Patrick wakikabidhi mafuta ya kupikia
Tunafuatilia kinachoendelea.......

Baada ya zoezi la kukabidhi misaada kumalizika-Wasanii kutoka MUCO Michael Onesmo na Gabriel wakiimba nyimbo maalum kwa watoto hao

Zoezi la kupiga picha za kumbukumbu likaendelea

Picha ya kumbukumbu

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com