Rais wa Burundi Pierre Nkurunziza
amewapongeza wanajeshi wazalendo waliozuia mapinduzi na kurejesha hali
ya usalama na utawala huru mjini Bujumbura.
Meja jenerali Godefroid Niyombare,aliyetangaza ''mapinduzi'' |
Rais Nkurunziza amewataka waburundi wazalendo kujitokeza kwa wingi katika uchaguzi utakaofanyika mwezi juni.
Rais
huyo alikuwa Mjini Dar es Salaam Tanzania siku ya Jumatano kuhudhuria
mkutano wa viongozi wa kanda ya Afrika Mashariki kundi la wanajeshi
waasi walipotangaza ''Mapinduzi'' dhidi ya serikali yake.
Rais Nkurunziza |
Viongozi
watatu miongoni mwa makamanda6 wa jeshi waliounga mkono tangazo hilo
la ''mapinduzi'' ilikupinga muhula wa tatu wa rais huyo tayari
wamekamatwa.
Kufikia sasa watu 105,000 wameripotiwa kutorokea mataifa jirani kulingana na takwimu za Umoja wa Mataifa.
Baada
ya kurejea kutoka Tanzania rais Nkurunzinza alielekea Kaskazini mwa
Bujumbura eneo alikotokea kabla ya kurejea katika kasri la rais lililoko
katika mji mkuu wa Bujumbura.
Katika taarifa iliyochapishwa mtandaoni rais Nkurunzinza alisema kuwa ''
Kuna
amani na utangamano katika asilimia kubwa ya Burundi na hata katika mji
mkuu wa Bujumbura ila tu watu wachache waasi ndio waliokuwa na hamu ya
kuvuja damu''
''Jeshi la taifa lilionesha ukomavu wake lilipokabiliana na wasaliti hao''
''Ningependa kuwahimiza waburundi wazalendo walinde kwa dhati amani
iliyoko sasa kwani ndio ngao na msingi wa demkrasia iliyoko Burundi''
''Shari msingi wa demokrasia yetu changa ilindwe isiyeyuke''
Nkurunziza aliahidi kulipiza kisasi dhidi ya ''yeyote aliyejaribu kuwasha moto wa uhasama baina ya waburundi''
Rais Nkurunzinza aliwasili mjini Bujumbura Ijumaa akiwa ameambatana na maelfu ya wafuasi wake.
Wengi wao wafuasi wa chama chake ambao walimshangilia kwa kurejea kwake huko .
Mwandishi
wa BBC aliyeko huko Ruth Nesoba anasema japo asilimia kubwa ya mji huo
ulikuwa na amani, katika sehemu zingine kulikuwa na waandamanaji
walioweka vizuizi barabrani wakipinga kuwania kwake kwa muhula wa tatu.
Polisi wa kupambana na ghasia walikuwa wakikabiliana nao kwa kuwafyatulia mabomu ya kutoa machozi.
Miongoni mwa makamanda waliokamatwa kwa kuchochea uasi ni pamoja na waziri wa zamani wa ulinzi Cyrille Ndayirukiye.
Waziri wa sasa wa usalama Gabriel Nizigama aliiambia BBC kuwa
maafisa wawili wakuu katika idara ya polisi pia walikamatwa pamoja na
wadogo wao takriban 12 waliokuwa wakiwalinda.
Wawili hao walikamatwa baada ya ufyatulianaji wa risasi nje ya jumba walimokuwa.
Kiongozi
wa uasi huo meja jenerali Godefroid Niyombare,aliyetangaza
''mapinduzi'' hayo siku ya jumatano hajakamatwa japo alinukuliwa na
shirika la habari la AFP akisema kuwa atajisalimisha.
''Nitajisalimisha kwa utawala, natumai hawataniua'' alisema meja jenerali Niyombare.
Via>>BBC
Via>>BBC
Social Plugin