Shilole |
Siku chache zikiwa zimepita tangu picha ambayo ilimuonyesha msanii Shilole kuwa wazi baadhi ya sehemu zake za juu akiwa stejini nchi ya Ubeligiji,Mei 14 Baraza la sanaa Tanzania(Basata) wameamua kutoa taarifa yao ambayo imetolewa na Katibu Mkuu Godfrey Mngereza,mtu wako wa nguvu barua hiyo imenifikia naomba kushare na wewe.
*******
"Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) ambalo ni msimamizi wa sekta ya
Sanaa na burudani nchini limeona picha chafu na zisizo na maadili za
Msanii Zuwena Mohamed maarufu kama Shilole alipokuwa akifanya onesho
lake nchini Ubeligiji hivi karibuni.
Katika picha hizo ambazo zimelaaniwa na watanzania wengi nchini
kupitia njia mbalimbali ikiwemo mitandao ya kijamii, Shilole anaonekana
akiwa Jukwaani huku viungo vyake vya sehemu za siri vikiwa hadharani na
zaidi akionesha tabia ambazo kwa kiasi kikubwa zimefedhehesha na
kuidhalilisha sekta ya Sanaa na Taifa kwa ujumla.
Aidha, BASATA limepokea malalamiko kwa njia ya simu na mawasiliano ya
internet kutoka kwa watanzania waishio ughaibuni wakilaani tukio la
Msanii huyo.
Katika mawasiliano yao wameeleza kwamba wamefedheheshwa na kudhalilika na tabia hiyo chafu iliyooneshwa na msanii huyu.
Katika mawasiliano yao wameeleza kwamba wamefedheheshwa na kudhalilika na tabia hiyo chafu iliyooneshwa na msanii huyu.
Ikumbukwe kwamba, Shilole ni msanii aliyesajiliwa na Baraza la Sanaa
la Taifa, hivyo anapokwenda nje ya nchi kabla hajapata visa anapewa
barua ya utambulisho kama msanii wa Tanzania, hivyo anapokuwa nje ya
nchi anatambuliwa kama msanii Mtanzania, anapofanya kinyume na misingi
ya kazi ya Sanaa, anajifedhehesha yeye mwenyewe, kazi ya Sanaa na nchi
yetu pia.
Aidha, ikumbukwe kwamba BASATA limeshapata kumwita na kumuonya msanii
huyu kutokana na tabia yake ya kutokujiheshimu pale awapo jukwaani na
yeye aliahidi kubadilika na kuachana na tabia hiyo chafu.
Kwa hiyo kuendelea kwake kufanya matukio hayo na kwa sasa katika ardhi ya nchi nyingine ni uthibitisho kwamba hajabadilika na kwa maana hiyo ameendelea kuidhalilisha Sanaa na wasanii wa kitanzania wenye kujitambua na kuiheshimu Sanaa kama kazi nyingine.

BASATA linapenda kueleza kwamba;
- Litamuita kwa mara nyingine tena kumtaka ajieleze kwa nini alifanya onesho hilo la kujidhalilisha na kudhalilisha hadhi ya mwanamke, msanii na Sanaa kwa ujumla.
- Kama maelezo yake hayataridhisha hatua kali za kinidhamu zitachukuliwa dhidi yake maana tayari ameshadhihirisha kwamba akifanyacho si Sanaa na hakina uhusiano na kazi ya Sanaa ambayo ina heshima yake na inahitaji ubunifu, weledi na kujitambua
BASATA linawakumbusha wasanii wote nchini kuwa Sanaa ni kazi kama
kazi zingine lakini siku za hivi karibuni wasanii wengi wamekuwa
wakikiuka suala zima la maadili kwa kutengeneza kazi chafu zisizofaa
mbele ya jamii ya watanzania wanaoipenda na kuiheshimu kazi ya Sanaa
yenye staha.
Tuungane kwa pamoja kukemea kazi chafu zinazozalishwa na wasanii wasiojitambua kwani suala la maadili ni suala mtambuka na linaanzia katika ngazi ya familia.
Tuungane kwa pamoja kukemea kazi chafu zinazozalishwa na wasanii wasiojitambua kwani suala la maadili ni suala mtambuka na linaanzia katika ngazi ya familia.
Aidha, BASATA linawataka Wasanii wote nchini kufuata sheria, kanuni
na taratibu mara wanapopata mialiko ya kikazi kwenda nje ya nchi.
Linawakumbusha kwamba haiwezekani msanii kutumia picha chafu na mavazi dhalili na kuonyesha utupu katika kuvuta mashabiki.
via>>Millardayo.com
Linawakumbusha kwamba haiwezekani msanii kutumia picha chafu na mavazi dhalili na kuonyesha utupu katika kuvuta mashabiki.
via>>Millardayo.com