Si jambo la kawaida kusikia mtoto kamuua mama yake ama mama kamuua mtoto wake, japo kwa miaka ya sasa matukio kama hayo yameshamiri kwa kiasi kikubwa sehemu mbalimbali duniani.
Tukio la mtoto kumuua mama yake leo limechukua headlines huko Zimbabwe baada ya kutokea kutoelewana baina yao.
Kilichotokea ni kwamba binti wa miaka 17 amemuua mama yake kwa kumchoma moto baada kulazimishwa kufua nguo chafu, kitendo kilichomkasirisha na kufikia uamuzi huo.
Kabla ya kumuua mama yake kwa kumwagia mafuta kisha kumchoma moto, mama yake alimpiga kitendo kilichomuuzi binti huyo na kufanya uamuzi huo mgumu.
Polisi wamemfungulia mtoto huyo mashtaka ya mauaji licha ya kupewa taarifa kuwa alikua akisumbuliwa na ugonjwa wa akili.
Social Plugin