Mtu
moja amepatikana akiwa amefariki dunia kati ya watu watatu walio
zama baharini baada ya kupinduka na FAIBA BOT huko Wesha katika wilaya Chake Chake huku ikiwa watu wawili bado kupatikana hadi zoezi la uokozi
lilipo fungwa rasmi hivi leo.
Wakitangaza kufunga kwa zoezi hilo uongozi wa Mkoa Kusini Pemba
kamanda wa polisi mkoa Kusini Pemba Juma Yusufu Ali na mkuu wa mkoa huo
Bimwana Juma Majid Abdalla walio kuwepo eneo la tukio wamesema kazi ya uokozi ilikwenda kwa kasi na kufanikiwa kupata mtu moja
akiwa amekwisha fariki huko bandarini Mkumbuu .
Wamemtaja aliyepatikana kuwa ni Ali Mbarouk Salehe (55) mkazi wa Mitamani Chake Chake na wale ambao bado hawaja onekana kuwa ni Rashid
Zahor na Omar Najimu Kibete wote wakaazi wa Mkoroshoni.
Akizungungumzia tukio hilo mmoja wa manusura wa ajali hiyo aliye
kuwemo ndani ya boti hiyo Ahmed Nasor 5(2) amesema jitihada za kutaka
kuwaokoa wenzao hao ilifanyika ila kwa vile hakukuwa na chombo karibu ndiyo
ilipelekea wenzao hao kupotea.
Naye moja wa waokozi amesema
wamefanikiwa kupata vifaa walivyokuwa navyo watu hao baada ya kuzamia
katika boti yao ambayo ipo chini ya bahari na walipoikagua hakuna mtu
hata moja.
Jitihada kubwa za kuwatafuta ilifanyika katika mwambao wa bahari ya
eneo la Pemba Chanal walipozama watu hao kwa kutumia boti ngalawa
watembea kwa miguu kwenye mikoko na ndenge aina ya chata ambayo
imezunguka hadi mwambao wa Tanga.
Via>>ITV