Chama
cha Demokrasia na Maendeleo -Chadema kimefanya mkutano mkubwa wa
hadhara katika viwanja vya Kawe jijini Dar es Salaam kwa lengo la
kuzindua rasmi mpango uitwao FTP 200 uliolenga kuhakikisha kila kata
kinakuwa na walinzi 200 wa chama hicho.
Akizungumza katika uzinduzi huo mwenyekiti wa Chadema Freeman Mbowe
amesema moja kati ya mambo ya msingi ambayo kwa sasa yanatakiwa
kufanyika ni tume ya taifa ya uchaguzi kuhakikisha zoezi la uandikishaji
wapiga kura linafanyika kikamilifu la sivyo watabeba mzigo wa lawama.
Social Plugin