Vichwa vya habari magazetini, kwenye
radio na TV kwa siku mbili mfululizo ilikuwa ishu ya mgomo wa madereva
wa mabasi ya abiria.. jana mchana Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda
akafika kituo cha Mabasi Ubungo akaongea na madereva na kuwaahidi
kushughulikia hii ishu, mgomo ukaisha safari za mabasi zikaendelea kama
kawaida.
Leo kaja na majibu kuhusu kile ambacho
Serikali imeamua kuhusu kushughulikia kero mbalimbali za madereva
zilizofanya wakafanya mgomo; >>
Tumekaa
jana na ahadi yangu imetimia.. niliahidi ya kwamba kama kile kikao
hakitakuwa na majibu ambayo ndugu zangu madereva wanayataka mimi
nitatangaza mgomo leo, lakini jana nimekutana na Waziri wa Uchukuzi,
Waziri wa Mambo ya Ndani, Waziri wa Kazi, Naibu Waziri wa Fedha,
SUMATRA, TABOA , TATOA na Afande Mpinga.. Chini ya Waziri Mkuu wameunda Kamati ambayo itashughulika na kero zote za usafiri na ni Kamati ya Kudumu>>– DC Paul Makonda.
>>Madereva
watakua na watu watano wa kuwawakilisha kwenye hicho.. nina uhakika
kwamba chombo hiki kitajibu kero zao.. Kamati hii ni ya kudumu kwa kuwa
hatujui kesho kuna kero gani itatokea.. lengo ni kutatua changamoto zote
za usafiri nchini kwa muda wote badala ya kusubiri mgomo utokee ndiyo
tuanze kutafuta majibu>>– DC Makonda.
“Watu wengi hawapendi watu wasiowapenda wafanye mambo mazuri.. Mkuu wa Wilaya kama alipigwa mawe basi Mkuu wa Wilaya huyu Makonda ni mkubwa kuliko hata mawe, waliokuwa wakimpiga mawe walikubali vipi kumsikiliza wakaweka mawe pembeni.. mimi sikupigwa mawe“>>–DC Paul Makonda.
Majibu hayo ya Paul Makonda utayasikia pia kwenye hii sauti hapa, bonyeza play
Social Plugin