Mmoja wa wazee wanaolelewa katika kituo cha Kolandoto katika manispaa ya Shinyanga |
Choo kilichojengwa na kampuni ya Easyflex Production ya Shinyanga mjini kwa ajili ya wazee wanaolelewa katika kituo cha Kolandoto katika manispaa ya Shinyanga Mkurugenzi wa EASY FLEX PRODUCTION Bi. Happiness Kihama akiwa eneo la choo hicho Meya wa manispaa ya Shinyanga Gulam Hafeez Mukadam akizungumza baada ya kuzindua choo hicho Maneno yanayosomeka katika choo hicho Hawa ni baadhi ya wazee wanaolelewa katika kituo cha Kolandoto Shinyanga |
Haya ni magodoro 60 yaliyokabidhiwa na Easyflex Production kwa wazee wa Kolandoto,ikiwa ni msaada ulitolewa na Mgodi wa dhahabu wa Buzwagi uliopo Kahama unaomikiwa na kampuni ya uchimbaji madini ya ACACIA ambao waliahidi kuwasaidia wazee hao wakati wa harambee iliyoendeshwa na Easyflex Production mwaka jana |
Baada ya wazee wanaoishi katika kituo cha makazi ya wazee wasiojiweza cha Kolandoto manispaa ya Shinyanga kulalamika kwa muda mrefu kutokana na tatizo sugu la ukosefu wa choo na kulazimika kutembea umbali mrefu kutafuta huduma hiyo vichakani hatimaye tatizo hilo limepatiwa ufumbuzi kwa kujengewa choo na Kampuni ya Uzalishaji na usambazaji wa Video na sauti EASY FLEX PRUDUCTION ya mjini Shinyanga.
Akitoa taarifa ya mradi wa ujenzi wa choo hicho na kukabidhi msaada wa viti 30 na magodoro 60 kwa ajili ya malazi ya wazee hao vyenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 20 mkurugenzi wa EASY FLEX PRODUCTION Bi. Happyness Kihama amesema kampuni yake imeamua kuwajengea choo na kutoa msaada huo kutokana na kuguswa na matatizo yanayowakabili wazee hao kituoni hapo ikiwa pia ni kuwaepusha na magonjwa ya mlipuko kutokana na kujisaidia hovyo.
Kihama amesema msaada wote uliotolewa unathamani ya sh 21.7 milioni ikiwa ni michango ya wadau mbalimbali, iliyotolewa kupitia harambee ambayo iliratibiwa na asasi hiyo katika kusaidia kambi ya wazee na kituo cha watoto wenye ulemavu jumuisha cha Buhangija.
“Bado kuna changamoto kubwa katika kuielimisha jamii umuhimu wa kusaidia wenye mahitaji maalumu ,nawaomba wananchi na watanzania wenzangu tubadilike tusaidie makundi haya kwani hayana msaada mwingine zaidi yetu sisi wanajamii na tusiiachie serikali pekee haiwezi kutekeleza kila jambo “amesema Kihama.
Akipokea
msaada huo na jengo la choo chenye matundu manne kwa niaba ya mkuu wa
mkoa wa Shinyanga Bw. Ally Rufunga mstahiki meya wa manispaa ya
shinyanga Bw. Gullam Hafidh Mukadam pamoja na kuishukuru taasisi hiyo ameitaka
jamii ya watanzania kuwa na mwamko wa kuanza kuwasaidia wazee na watu
wenye mahitaji maalum badala ya kusubiri misaada kutoka kwa wahisani wa
nje ya nchi hali ambayo imekuwa ikidhalilisha utu wa mtanzania.
Kwa
upande wao mlezi msaidizi wa kituo hicho Evodia Ndaka na
mwenyekiti wa makazi hayo Simon Maganga wameiomba serikali kuzifanyia
ukarabati mkubwa nyumba za makazi hayo ya wazee kutokana na majengo yake
kuchakaa hali inayowafanya waishi kwa wasiwasi mkubwa na kwamba
wamekuwa wakilazimika kuzihama wakati wa mvua inaponyesha kutokana na
kuvuja huku nyingi kati ya hizo tayari sehemu za kuta zake zimebomoka.
Hivi sasa kuna wazee 45 na watoto 16 wanaoishi katika kambi ya wazee wakoma ya Kolandoto manispaa ya Shinyanga
Hivi sasa kuna wazee 45 na watoto 16 wanaoishi katika kambi ya wazee wakoma ya Kolandoto manispaa ya Shinyanga