Kila mtu ana ndoto na mtu ambaye
anamhitaji awe mpenzi wake kwa maisha yote, sio ajabu mtu akawa na ndoto
za kumuwaza mtu ambaye ni ngumu sana kwenye mazingira ya kawaida kuonana
nae, pata picha ya huyu jamaa ambaye yeye macho na akili yake ni kwa Malia Obama.
Kiprono Matagei kazi yake ni wakili Kenya, ndoto yake ni yeye na Malia Obama damdam,
alianza kumpenda tangu mwaka 2008.. moyoni mwake akaweka ahadi kwamba
hatokuwa na uhusiano na mwanamke yoyote mpaka siku ampate Malia wake !!
Jamaa kajiongeza kabisa, amesema mahari aliyopanga kutoa ni hii>>> ng’ombe 50, kondoo 70 na mbuzi 30.
Kiprono kasema yuko serious kabisa na aliwashirikisha familia yake, wako tayari nao kumsaidia mpaka afanikiwe !!
Obama
atakuwa Kenya mwezi wa saba, ziara yake haitachukua muda mrefu lakini
jamaa amesema atajitahidi aitumie nafasi hiyo hiyo kumuona ‘baba mkwe
huyo mtarajiwa’ !!