Tukio hilo limetokea mchana eneo la Tabata TOT, baada ya gari hilo kugongwa kwa nyuma na lori na kupinduka.
Kutokana na ajali hiyo, kundi la vijana lilivamia na kuchukua chupa za bia huku wengine wakinywa mfululizo.
Mwandishi wa gazeti hili aliyekuwa eneo la tukio
alishuhudia vijana hao wakiwamo madereva wa bodaboda, wa magari makubwa
na wapita njia wakiokota chupa za bia hizo na kunywa.
Tukio hilo la aina yake, lilidumu kwa takribani 20
kabla ya polisi kuongeza nguvu kutoka askari wawili waliokuwa eneo hilo
wakizuia watu kuchukua chupa.
Vijana walionekana kuhatarisha usalama wao kwa
kuingia mitaroni ambako bia zilingukia humo na kuzichukua bila kujali
kuwa zimepasuka.
Vijana wengine walionekana kuanza kulewa kwa kunywa bila kipimo.
Dereva wa Fuso hilo, kutoka Kampuni ya Mwanahela,
Mohamed Said alisema mzigo huo wa bia aliutoa katika Kiwanda cha
Serengeti kwenda Kituo cha Polisi Mkoa wa Pwani.
“Hizi bia zilikuwa katika masanduku 500, ni mali
ya Polisi Pwani, ajali hii ni uzembe unaoonekana wazi kuwa wa dereva wa
lori, hata polisi wakija kupima watajua nani mwenye kosa,” alisema Said
kabla ya Fuso lingine kufika na kuchukua bia hizo na kuondoka nazo.
Mashuhuda wa tukio hilo walisema chanzo cha ajali
hiyo ni uzembe wa dereva wa lori aliyekuwa akitokea njia ya pembeni
kuingia barabara kuu bila tahadhari.
Hata hivyo, Dereva wa lori hilo, Godfrey Baregu
alisema kosa lilisababishwa na uzembe wa dereva wa Fuso ambaye alitakiwa
kusubiri ili yeye (Baregu) apite.
Na Kelvin Matandiko-Dar es salaam
Na Kelvin Matandiko-Dar es salaam
Social Plugin