Mkuu wa Mkoa wa Simiyu elaston Mbwilo akiongea na wananchi katika wilaya ya Meatu. |
Idadi ya wagonja ambao wameugua ugunjwa wa ajabu
uliozikumba jumla ya kata 6 katika wilaya ya Meatu Mkoani Simiyu imezidi
kuongezeka kila mara, tangu kuripotiwa kutokea kwa ugonjwa huo wiki mbili
zilizopita.
Mpaka jana taarifa zilizotolewa na Mganga Mkuu wa
wilaya ya Meatu Adamu Jimisha alisema kuwa idadi hiyo imeongezeka kutoka
wagonjwa 80 hadi kufikia 1048 ambao walifikishwa katika kituo cha afya
Mwandoya.
Jimishi alitoa taarifa hiyo mbele ya kamati ya
ulinzi na usalama ya Mkoa, iliyokuwa ikiongozwa na Mkuu wa Mkoa Erasto Mbwilo,
alipowatembelea baadhi ya wagonjwa waliokuwa wamelazwa katika kituo
hicho cha afya pamoja na kata za, Mwabusalu, Lingeka, Mwakisandu, Tindabuligi,
Pamoja na Lubiga ambazo zimekubwa na janga hilo.
Alieleza kuwa bado dalili za baadhi ya wagonjwa
ambao wamekuwa waliletwa katika kituo hicho cha afya tangu kutokea kwake,
zimekuwa ni zile zile kuumwa kichwa, kikohozi kikavu, mwili kulegea,
kuchanganyikiwa akili pamoja na kupoteza fahamu.
Aliongeza kuwa wagonjwa hao wamekuwa
wakitibiwa na kuruhusiwa kwenda nyumbani pindi wanapopata nafuu au kupona
kabisa, huku akibainisha kuwa baadhi yao walikutwa na magonjwa mbalimbali kama
malaria na minyoo.
Mganga Mkuu huyo alieleza kuwa wataalam wa Wizara
ya Afya na Ustawi wa Jamii wakiambatana na Timu ya Mkoa akiwemo Mganga Mkuu wa
Mkoa, Mtaalam wa Maabara na Daktari mmoja walichukua sampuli kwa ajili ya
kupeleka Nairobi kwa Uchunguzi.
Alisema timu hiyo ilipeleka vipimo hivyo tarehe
15/05/2015 kwa ajili ya kubaini aina gani ya ugonjwa, ambapo majibu alieleza
kuwa timu hiyo iliahidi kutoa mwishoni mwa mwezi huu.
Kwa upande wake mkuu wa Mkoa aliwataka wananchi wa
Wilaya hiyo waliokuwa wamefika kuwajulia hali baadhi ya wagonjwa katika kutoa
hicho cha afya kuwapeleka mapema hospitali watu watakaoonekana kuwa na dalili
za ugonjwa huo.
“ Msiiwaache wagonjwa majumbani waleteni na
msiwapeleke kwa waganga wa kienyeji,
mkiona watu wenye dalili za ugonjwa kama walivyowaeleza wataalam
waleteni haraka hapa Mwandoya wapatiwe matibabu” ,alisema Mbwilo.
Mbwilo aliwaeleza wananchi kuwa kwa mujibu wa
Watalaam wa Afya ugonjwa huo hauna
madhara ya kifo, hivyo akawataka kuendelea na shughuli zao kama kawaida wakati
Serikali inaendelea kufanya uchunguzi juu ya chanzo cha ugonjwa huo.
Nao baadhi ya wananchi wakiongea mbele ya mkuu
huyo wa Mkoa waliiomba Serikali kufuatilia haraka matokeo ya vipimo
vilivyochukuliwa na Wataalam hao ili wajue chanzo cha ugonjwa huo ambao mpaka
sasa hawaujajulikana.
“Tunaomba
majibu ya vipimo vilivyochukuliwa yaletwe haraka, maana mpaka sasa hivi hatujui
huu ni ugonjwa gani na chanzo chake nini, Serikali itusaidie katika hili”
alisema mmoja wa wananchi alijulikana kwa jina la Joseph.
Mhe Mbwilo alisema Serikali inaendelea kufuatilia
majibu ya vipimo hivyo vilivyochukuliwa na Timu ya Wataalam wa Afya kutoka Mkoa wa Simiyu na Wizara ya Afya na
Ustawi wa Jamii baada ya kukamilisha
taarifa zitatolewa kwa wananchi.
Via>>Simiyunews blog