Idadi
kubwa ya wanawake wanaofanya biashara ya ngono Mjini Kahama wamedaiwa kugoma
kutumia dawa ya kupunguza makali ya virusi vya ukimwi licha ya kupima na
kubainika wanaishi na maambukizi ya ugonjwa huo badala yake hutumia kula nyama
ya kitimoto kwa madai inapunguza kasi hiyo kuliko dawa za ARV.
Hali hiyo
imeelezwa jana Mjini Kahama na afisa maendeleo ya jamii Mjini Kahama Fanuel
Ruben ambaye amesema ofisi yake imefanya ukaguzi kwenye madanguro yanayotumiwa
na wanawake hao kwa biashara ya ngono na kubaini wapo wasichana kati ya miaka
15 hadi 20.
Ruben
amesema baada ya kubaini hiyo wamewachukua wasichana na kuwafanyia vipimo wengi
wao wamebainika kuwa na ujauzito na maambukuzi ya virusi vya ukimwi hali
iliyoonyesha wanafanya ngono bila kutumia kinga ya maambukizi ya magonjwa ya
kuambukiza.
Hata
hivyo amesema wasichana hao baada ya kuwafanyia uchunguzi wamegoma kutumia dawa
za kupunguza makali kwa madai wenzao wanaoishi na virusi vya ukimwi hutumia
nyama ya kitimoto badala ya dawa hiyo.
Kufuatia
hali hiyo Ruben amesema ameandaa mkakati wa kuwachukulia hatua wale wote
wanaofanya biashara ya ngono huku wakijua wao ni waathirika wa ugonjwa huo kwa
kuwa ipo sheria mpya inayokataza mwathirika wa virusi vya ukimwi kuwaambukiza
wenzake kwa makusudi.
Kauli
hiyo imekuja baada ya mkuu wa Wilaya ya Kahama Benson Mpesya kutangaza msako wa
kuyafunga madanguro yote yanayotumiwa na wanawake hao kwa biashara ya ngono
baada ya kubainika wengi wa wateja wao ni vijana wadogo ambao wanahatarisha
maisha yao.
Via>>Kijukuu Blog
Via>>Kijukuu Blog