Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

HII HAPA ORODHA YA MASTAA WA HIP HOP WENYE PESA NYINGI ZAIDI DUNIANI


Ripoti ya Forbes mwaka 2014 ilionesha P Diddy ameongoza kwenye list ya mastaa wa Hiphop wenye utajiri mkubwa zaidi, akafuatia Hiphop star Dr. Dre, #3 akakaa Jay Z, #4Birdman na #5 alikuwepo 50 Cent.. imetoka ripoti mpya, yes kuna mabadiliko kwenye hiyo list mtu wangu.

Mpangilio wenyewe mwaka 2015 ni huu hapa.

No.5: Rapper Birdman, mmoja ya members wa YMCMB. Utajiri wake kwa sasa unaonekana ni kama dola Mil. 150 hivi. Mwaka 2014 alikuwa nafasi ya nne kwa utajiri wa dola 160, ni kama biashara ya muziki bado haijawa vizuri kwa upande wake mwaka huu.

No.4: Rapper 50 Cent yuko namba nne, utajiri wake ni dola Mil.155. Ripoti ya mwaka 2014 ilionesha alikuwa nafasi ya 5 na utajiri wake ulikuwa dola Mil. 140, kapanda nafasi moja juu yani !!

No.3: YES YES !! Ni Jay Z mtu wangu, mwaka jana alikuwa nafasi hiyo hiyo ya tatu, utajiri wake ulikuwa sawa na dola Mil. 550 na mwaka huu kiwango ni hicho hicho. Jamaa ni mfanyabiashara wa ukweli, labda tusubiri kuona account zake benki zikituna zaidi baada ya kuzindua biashara ya Tidal !!

No.2: Dr. Dre, jamaa ni rapper, producer na mjasiriamali pia !! Biashara ya headphone za ‘Beats by Dre’ ni kitu kingine kikubwa kilichomuingizia pesa nyingi sana kabla hajauza mradi huo kwa Kampuni ya Apple. Utajiri wake ni dola Mil. 700, mwaka jana alikuwa dola Mil.550

No.1: Hajatoka kwenye hii nafasi ya kwanza ambayo hata mwaka 2014 alikuwa hapo pia, jamaa anabadilisha majina kila wakati !! Diddy ana utajiri wa dola Mil.735.. mwaka jana alikuwa na utajiri wa dola Mil.700.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com