Nje ya banda hilo |
Wakazi wa Shinyanga wakisubiri huduma nje ya banda la shirika la Intrahealth international |
Zaidi ya wanaume 315,000 wamefanyiwa tohara ya wanaume kwa
ajili ya kujikinga na Virusi vya UKIMWI katika mikoa ya Shinyanga, Simiyu na
wilaya ya Rorya mkoani Mara ikiwa ni sawa na asilimia 39 ya wanaume wanaoishi
katika mikoa hiyo miwili na wilaya ya Rorya.
Haya yamebainishwa jana na mganga mkuu wa mkoa wa Shinyanga
Dkt Ntuli Kapologwe baada ya Malunde1 blog kutembelea banda la shirika la Intrahealth International wakati wa ufunguzi wa maadhimisho ya siku ya Wauguzi
duniani yaliyofanyika kitaifa mkoani Shinyanga.
Dkt Kapologwe alisema huduma ya tohara imekuwa ikitolewa na watumishi wa idara ya afya waliopewa mafunzo maalumu na kati ya wahudumu hao wamo wauguzi.
Dkt Kapologwe alisema huduma ya tohara imekuwa ikitolewa na watumishi wa idara ya afya waliopewa mafunzo maalumu na kati ya wahudumu hao wamo wauguzi.
Dkt Kapologwe alisema idadi hiyo ya wanaume waliotahiriwa
imepatikana tangu serikali kwa kushirikiana na Intrahealth International kuanza
kutoa huduma ya tohara ya mwanaume kwa ajili kujikinga na VVU mwaka 2011.
“Wauguzi wametoa mchango mkubwa sana katika kufanikisha
kampeni ya kitaifa ya tohara ya mwanaume kwa ajili ya kujikinga na UKIMWI,”
alisema mganga mkuu wa mkoa wa Shinyanga, Dr. Ntuli Kapologwe.
Kwa mujibu wa Dr.
Kapologwe wauguzi wanawakilisha zaidi ya asilimia 55 ya watumishi wote wa idara
ya afya, hivyo uwepo wao ni msaada mkubwa kutatua changamoto za utoaji huduma
ya afya.
“Kwa kuwapa mafunzo ya utoaji wa huduma ambazo kitaaluma si
kazi yao tumeweza kutoa huduma kwa wananchi katika maeneo na vituo ambako kada
kama famasia ama madaktari hawapo,” alisema Dkt. Kapologwe.
Kwa upande wake mratibu wa huduma za UKIMWI mkoani Shinyinga
Dkt. Mawazo Amri alisema Kutokana ufadhili toka serikali ya marekani kupitia
mfuko wa rais wa marekani wa kudhibiti UKIMWI (PEPFAR) idara ya Marekani ya
Tiba na Udhibiti wa Maradhi (CDC) huduma ya tohara imeweza kufikishwa hadi
kwenye maeneo ya vijijini ambako kwa kawaida hakuna wahudumu wa afya wa kutosha
wenye ujuzi wa kufanya tohara.
“Kupitia kamati ya afya ya mkoa na kamati za afya za kila
wilaya na IntraHealth tunasambaza huduma ya tohara kwenye vituo vya afya vya
pembezoni na hivyo kuhakikisha kuwa kila
mwanaume ambaye anaihitaji huduma hii anaipata, alisema Dkt Amri.
Alisema serikali ya Tanzania ilianzisha kampeni ya kufanya
tohara ya mwanaume kwa jamii ambako hazikuwa na mila ya tohara baada ya
kuthibitika kisayansi kuwa tohara ya mwanaume inapunguza kwa asilimia 60
uwezekano wa mwanaume aliiyefanyiwa tohara kuambukizwa VVU.
Dkt Amri alisema tohara ya mwanaume, zaidi ya kuongeza
usafi, pia inachangia kupunguza uwezekano wa mwanamke ambaye mwenzi wake
ametahiriwa kupata saratani ya shingo ya uzazi.
Mkoa wa Shinyanga ni miongoni mwa mikoa yenye ushamiri
mkubwa wa maaumbikizi ya UKIMWI na idadi ndogo ya wanaume ambao wamefanyiwa
tohara, kwa mujibu wa takwimu za viashiria vya malaria na UKIMWI za mwaka 2011/2012.
Mikoa mingine ambayo imekuwa ikifanya jitihada kusambaza
huduma ya tohara ya mwanaume ni Njombe, Geita, Mbeya na Rukwa.
Idadi ya wanaume waliokwisha fanyiwa tohara inakaribia nusu
ya idadi ya wanaume wanaoishi katika mkoa wa Shinyanga na Simiyu.
Huduma ya tohara ya mwanaume inatolewa kwa aushirikiano kati
ya serikali ya Tanzania kupitia wizara ya afya na ustawi wa jamii na wanau wa
maendeleo yaani shirika la Intrahealth International ambalo hufanya program
mbalimbali za afya zenye kuweka mbele utendaji wa wafanyakazi wa idara ya afya.
Siku ya wauguzi kitaifa inaadhimishwa kitaifa mjini Shinyanga
ikiwa na kauli mbiu isemayo wauguzi kiini cha mabadiliko; huduma bora za afya
kwa gharama nafuu ambapo kilele chake ni leo Mei 12,2015 lakini huduma ya tohara itaendelea kutolewa hadi Mei 16 mwaka huu
katika viwanja vya Shycom.
Na Kadama Malunde-Shinyanga
Social Plugin