Nchi nyingi duniani zimekuwa zikikabiliana na matumizi ya bidhaa feki ikiwemo vyakula na vipodozi ambavyo kwa kiasi kikubwa huathiri afya za watumiaji.
Huko Uingereza imeelezwa kuwa kinyesi cha panya na mkojo ni baadhi ya viungo vinavyotumika kutengeneza bidhaa feki za urembo kwa wanawake.
Utafiti wa bidhaa za urembo zinazouzwa kwa njia ya mtandao nchini Uingereza umebaini kuwa bidhaa hizo zina tengezwa kwa njia isiyofUata maadili na kulinda afya za binadamu ikiwemo marashi na mafuta ya kujipaka.
Kwa mujibu wa Polisi waliofanya uchunguzi huo, wamedai mfumuko wa bei ya bidhaa kwa njia za kielektroniki umechangia ongezeko la mauzo ya bidhaa hizo.
Social Plugin