Stori ambazo zimewahi kuripotiwa na baadhi ya vyombo vya habari na
kuingia kwenye headlines mbalimbali ni zile ambazo tunasikia mara kwa
mara kuwa Daktari alikuwa anafanya Operesheni(Upasuaji) lakini kwa bahati
mbaya akasahau mkasi au akasahau baadhi ya vifaa vingine vya Matibabu.
Leo stori ambayo nashare na wewe mtu wangu ni kuhusu Daktari ambaye
alisahau simu yake ya mkononi kwenye tumbo la Mama Mjamzito baada ya
kufanyiwa upasuaji,ambaye alienda kujifungua na huyo daktari ndiye
aliyekua akiongoza Upasuaji huo kwa huyo mama.
Hii imetokea kwenye nchi ya Jordan na inasemwa kuwa Mama huyo
aligundua hali hiyo baada ya simu hiyo kuanza kuunguruma tumboni,Taarifa
ya Gulf News inasema mwanamke huyo anatmabulika kwa jina la Hanan
Mahmood Karim ambaye ana umri wa miaka 36, alijifungua mtoto wa kiume
akiwa na uzito wa Kg 4.8
Social Plugin